Surat Al-Qamar (القمر) ni sura ya 54 katika Qur’ani na ina aya 55. Jina lake lina maana ya “Mwezi”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 27.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Qamar yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Qamar kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
ٱقْتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلْقَمَرُ١
Iqtarabati alssaʿatu wainshaqqa alqamaru
Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!1
Maelezo
[1] Kiyama kimekaribia na mwezi utapasuka hapana hivi wala hivi. -
وَإِن يَرَوْا۟ ءَايَةً يُعْرِضُوا۟ وَيَقُولُوا۟ سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ٢
Wain yaraw ayatan yuʿridoo wayaqooloo sihrun mustamirrun
Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.2
Maelezo
[2] Na makafiri wakiona Ishara, yaani muujiza mkubwa, wao hupuuza wakaacha kuuamini. Bali husema: Huu ni uchawi wa daima unaendelea! -
وَكَذَّبُوا۟ وَٱتَّبَعُوٓا۟ أَهْوَآءَهُمْ ۚ وَكُلُّ أَمْرٍ مُّسْتَقِرٌّ٣
Wakaththaboo waittabaʿoo ahwaahum wakullu amrin mustaqirrun
Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.3
Maelezo
[3] Na wamewakanusha Mitume na wakafuata yaliyo zainishwa na matamanio yao. Na kila jambo huishia mwisho wake linapo tulia na kuthibiti. -
وَلَقَدْ جَآءَهُم مِّنَ ٱلْأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزْدَجَرٌ٤
Walaqad jaahum mina alanbai ma feehi muzdajarun
Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.4
Maelezo
[4] Na ninaapa kuwa zimewajia makafiri khabari za mataifa yaliyo tangulia zenye ukweli wa uumbaji ambazo zina mikemeo ya kutosha. -
حِكْمَةٌۢ بَـٰلِغَةٌ ۖ فَمَا تُغْنِ ٱلنُّذُرُ٥
Hikmatun balighatun fama tughnee alnnuthuru
Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!5
Maelezo
[5] Haya yaliyo wajia ni hikima kubwa na lengo la kufikia mbali. Lakini maonyo yataleta faida gani kwa wanao zipinga hikima hizo? -
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ ۘ يَوْمَ يَدْعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَىْءٍ نُّكُرٍ٦
Fatawalla ʿanhum yawma yadʿu alddaʿi ila shayin nukurin
Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha; .6
Maelezo
[6] Ewe Muhammad! Waachilie mbali hawa makafiri, nawe ngojea siku atapoita mwitaji wa Mwenyezi Mungu kuitia jambo ambalo nafsi inalichukia mno! -
خُشَّعًا أَبْصَـٰرُهُمْ يَخْرُجُونَ مِنَ ٱلْأَجْدَاثِ كَأَنَّهُمْ جَرَادٌ مُّنتَشِرٌ٧
Khushshaʿan absaruhum yakhrujoona mina alajdathi kaannahum jaradun muntashirun
Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika!7
Maelezo
[7] Macho yao yatainamia chini kwa wingi wa kitisho, wakitoka makaburini kama kwamba ni nzige walio tawanyika, kwa wingi wao na mbio zao. -
مُّهْطِعِينَ إِلَى ٱلدَّاعِ ۖ يَقُولُ ٱلْكَـٰفِرُونَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَسِرٌ٨
Muhtiʿeena ila alddaʿi yaqoolu alkafiroona hatha yawmun ʿasirun
Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.8
Maelezo
[8] Wakimkimbilia huyo mwitaji, wakimtazama kwa unyonge na unyenekevu, macho yao yanamwangalia yeye tu. Makafiri watasema Siku ya Kiyama: Hii leo ni siku nzito, siku ya shida! -
۞ كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا۟ عَبْدَنَا وَقَالُوا۟ مَجْنُونٌ وَٱزْدُجِرَ٩
Kaththabat qablahum qawmu noohin fakaththaboo ʿabdana waqaloo majnoonun waizdujira
Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.9
Maelezo
[9] Kabla ya makafiri wa Makka walikwisha kanusha kaumu ya Nuhu. Walimkadhibisha Nuhu, mja wetu na Mtume wetu, wakamsingizia kuwa ana wazimu. Wakaingiza baina yake na kufikisha kwake Ujumbe kila namna ya maudhi na vitisho. -
فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَغْلُوبٌ فَٱنتَصِرْ١٠
Fadaʿa rabbahu annee maghloobun faintasir
Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!10
Maelezo
[10] Nuhu akamwomba Mola wake Mlezi akisema: Hakika mimi nimeshindwa na hawa watu wangu, basi wapatilize hawa kwa ajili yangu! -
فَفَتَحْنَآ أَبْوَٰبَ ٱلسَّمَآءِ بِمَآءٍ مُّنْهَمِرٍ١١
Fafatahna abwaba alssamai bimain munhamirin
Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika.11
Maelezo
[11] Basi tukaifungua milango ya mbingu ikamimina maji yasiyo katika; -
وَفَجَّرْنَا ٱلْأَرْضَ عُيُونًا فَٱلْتَقَى ٱلْمَآءُ عَلَىٰٓ أَمْرٍ قَدْ قُدِرَ١٢
Wafajjarna alarda ʿuyoonan failtaqa almao ʿala amrin qad qudira
Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa.12
Maelezo
[12] Na tukaipasua ardhi kwa chemchem zikitibuka maji. Yakakutana maji ya mbinguni na maji ya ardhi kuwahiliki, kama alivyo kadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu. -
وَحَمَلْنَـٰهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلْوَٰحٍ وَدُسُرٍ١٣
Wahamalnahu ʿala thati alwahin wadusurin
Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.13
Maelezo
[13] Tukampakia Nuhu katika jahazi la mbao zinazo fungwa pamoja kwa kamba, kama mtepe. -
تَجْرِى بِأَعْيُنِنَا جَزَآءً لِّمَن كَانَ كُفِرَ١٤
Tajree biaʿyunina jazaan liman kana kufira
Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.14
Maelezo
[14] Likawa linakwenda baharini chini ya hifadhi yetu, kuwa ni malipo kwa Nuhu ambaye watu wake waliendelea kuukanya wito wake. -
وَلَقَد تَّرَكْنَـٰهَآ ءَايَةً فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ١٥
Walaqad taraknaha ayatan fahal min muddakirin
Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka?15
Maelezo
[15] Na tumeliacha hilo tukio na kuzamishwa makafiri na kuokolewa Waumini liwe ni mawaidha, lakini yupo mwenye kuwaidhika? -
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ١٦
Fakayfa kana ʿathabee wanuthuri
Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.16
Maelezo
[16] Jee, vipi ilikuwa adhabu yangu na onyo langu kwa wakhalifu. -
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ١٧
Walaqad yassarna alqurana lilththikri fahal min muddakirin
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?17
Maelezo
[17] Ninaapa, tumeifanya Qur'ani iwe sahali kukumbukwa na kutoa mawaidha. Lakini je, yupo wa kuwaidhika? -
كَذَّبَتْ عَادٌ فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ١٨
Kaththabat ʿadun fakayfa kana ʿathabee wanuthuri
Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?18
Maelezo
[18] Kina A'di walimkadhibisha Mtume wao Hudi. Je, hali gani adhabu yangu na onyo langu lilikuwa kwa wendao kinyume! -
إِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِى يَوْمِ نَحْسٍ مُّسْتَمِرٍّ١٩
Inna arsalna ʿalayhim reehan sarsaran fee yawmi nahsin mustamirrin
Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo,19
Maelezo
[19] Sisi kwa yakini tuliwapatiliza kwa upepo ubaridi unao vuma, katika siku ya ukorofi wa daima, -
تَنزِعُ ٱلنَّاسَ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ مُّنقَعِرٍ٢٠
Tanziʿu alnnasa kaannahum aʿjazu nakhlin munqaʿirin
Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng'olewa.20
Maelezo
[20] Ukiwang'oa watu na kuwatupa nao wamekufa, kama vinavyo ng'olewa vigogo vya mitende na mizizi yake. -
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ٢١
Fakayfa kana ʿathabee wanuthuri
Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?21
Maelezo
[21] Hali gani adhabu yangu na onyo langu lilikuwa kwa walio kwenda kinyume! -
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ٢٢
Walaqad yassarna alqurana lilththikri fahal min muddakirin
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka?22
Maelezo
[22] Na bila ya shaka Sisi tumeifanya sahali Qur'ani kwa ajili ya mawaidha na mazingatio, basi je, yupo wa kuwaidhika? -
كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِٱلنُّذُرِ٢٣
Kaththabat thamoodu bialnnuthuri
Thamudi waliwakanusha Waonyaji.23
Maelezo
[23] Thamudi walikadhibisha maonyo ya Nabii wao, Saleh. -
فَقَالُوٓا۟ أَبَشَرًا مِّنَّا وَٰحِدًا نَّتَّبِعُهُۥٓ إِنَّآ إِذًا لَّفِى ضَلَـٰلٍ وَسُعُرٍ٢٤
Faqaloo abasharan minna wahidan nattabiʿuhu inna ithan lafee dalalin wasuʿurin
Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa!24
Maelezo
[24] Wakasema: Hivyo aje mtu tu katika sisi, watu wa kawaida, asiye na watu, nasi tumfuate? Tukimfuata huyo basi bila ya shaka sisi tutakuwa mbali mno na haki, na tutakuwa tuna wazimu basi. -
أَءُلْقِىَ ٱلذِّكْرُ عَلَيْهِ مِنۢ بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ٢٥
Aolqiya alththikru ʿalayhi min baynina bal huwa kaththabun ashirun
Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi!25
Maelezo
[25] Uteremshiwe wahyi kwake yeye katika sisi na hali wapo wanao stahiki zaidi? Bali huyo kazikdi katika uwongo, mwenye kukanya neema. -
سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَّنِ ٱلْكَذَّابُ ٱلْأَشِرُ٢٦
Sayaʿlamoona ghadan mani alkaththabu alashiru
Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.26
Maelezo
[26] Karibu watakuja jua siku itapo wateremkia adhabu ni nani mwongo anaye ikanya neema. Wao au Saleh, Mtume wao? -
إِنَّا مُرْسِلُوا۟ ٱلنَّاقَةِ فِتْنَةً لَّهُمْ فَٱرْتَقِبْهُمْ وَٱصْطَبِرْ٢٧
Inna mursiloo alnnaqati fitnatan lahum fairtaqibhum waistabir
Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili.27
Maelezo
[27] Hakika Sisi tunampelekea Mtume wetu Saleh ngamia mke, awe ni mtihani wao. Basi wangojee, na uwatazame watafanya nini. Na subiri, uvumilie maudhi yao mpaka itapo kuja amri ya Mwenyezi Mungu. -
وَنَبِّئْهُمْ أَنَّ ٱلْمَآءَ قِسْمَةٌۢ بَيْنَهُمْ ۖ كُلُّ شِرْبٍ مُّحْتَضَرٌ٢٨
Wanabbihum anna almaa qismatun baynahum kullu shirbin muhtadarun
Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika.28
Maelezo
[28] Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao na ngamia. Kila mmoja wao atakuwa na zamu yake aje kunywa katika siku yake. -
فَنَادَوْا۟ صَاحِبَهُمْ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ٢٩
Fanadaw sahibahum fataʿata faʿaqara
Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.29
Maelezo
[29] Wakamwita mtu wao mmoja akapania kumchinja yule ngamia, akamchinja. -
فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ٣٠
Fakayfa kana ʿathabee wanuthuri
Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!30
Maelezo
[30] Basi vipi ilikuwa adhabu yangu na onyo langu kwa hao wakhalifu walio kwenda kinyume na amri. -
إِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَكَانُوا۟ كَهَشِيمِ ٱلْمُحْتَظِرِ٣١
Inna arsalna ʿalayhim sayhatan wahidatan fakanoo kahasheemi almuhtathiri
Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa.31
Maelezo
[31] Sisi tuliwapatiliza kwa ukelele mmoja tu, wakawa kama miti mikavu anayo ikusanya yeyote atakaye kujengea boma la uwa wake. -
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ٣٢
Walaqad yassarna alqurana lilththikri fahal min muddakirin
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?32
Maelezo
[32] Na bila ya shaka Sisi tumeisahilisha Qur'ani iwe nyepesi kwa ajili ya mawaidha na kuzingatia. Lakini je, yupo wa kuwaidhika? -
كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍۭ بِٱلنُّذُرِ٣٣
Kaththabat qawmu lootin bialnnuthuri
Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji.33
Maelezo
[33] Kaumu Lut'i nao walikadhibisha maonyo ya Mtume wao. -
إِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ ۖ نَّجَّيْنَـٰهُم بِسَحَرٍ٣٤
Inna arsalna ʿalayhim hasiban illa ala lootin najjaynahum bisaharin
Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.34
Maelezo
[34] Hakika Sisi tuliwapelekea upepo mkali wa kuwatupia changarawe. Isipo kuwa watu wa Lut'i walio amini. Hao tuliwaokoa na adhabu hii mwisho wa usiku. -
نِّعْمَةً مِّنْ عِندِنَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى مَن شَكَرَ٣٥
Niʿmatan min ʿindina kathalika najzee man shakara
Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru.35
Maelezo
[35] Kwa kuwapa neema iliyo toka kwetu. Neema kama hizo kubwa kubwa ndivyo tunavyo walipa wenye kuishukuru neema yetu kwa imani yao na ut'iifu. -
وَلَقَدْ أَنذَرَهُم بَطْشَتَنَا فَتَمَارَوْا۟ بِٱلنُّذُرِ٣٦
Walaqad antharahum batshatana fatamaraw bialnnuthuri
Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo.36
Maelezo
[36] Na hakika Lut'i aliwahadharisha watu wake vipi mshiko wetu ulivyo mkali, wakatilia shaka maonyo yake kwa kuwa wanamwona mwongo. -
وَلَقَدْ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيْفِهِۦ فَطَمَسْنَآ أَعْيُنَهُمْ فَذُوقُوا۟ عَذَابِى وَنُذُرِ٣٧
Walaqad rawadoohu ʿan dayfihi fatamasna aʿyunahum fathooqoo ʿathabee wanuthuri
Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!37
Maelezo
[37] Wakamtaka awape wageni wake wawatende fiili yao, tukayafuta macho yao kuwa ni malipo kwa hilo walilo litaka. Basi waambie kwa kuwakejeli: Igugumieni adhabu yangu, na maonyo yangu! -
وَلَقَدْ صَبَّحَهُم بُكْرَةً عَذَابٌ مُّسْتَقِرٌّ٣٨
Walaqad sabbahahum bukratan ʿathabun mustaqirrun
Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.38
Maelezo
[38] Na asubuhi mapema ikawashitua adhabu ya kuthibiti milele. -
فَذُوقُوا۟ عَذَابِى وَنُذُرِ٣٩
Fathooqoo ʿathabee wanuthuri
Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!<39
Maelezo
[39] Wakaambiwa: Igugumieni adhabu yangu na maonyo yangu! -
وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ٤٠
Walaqad yassarna alqurana lilththikri fahal min muddakirin
Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka?40
Maelezo
[40] Na hakika tumeifanya Qur'ani ni sahali kwa ajili ya mawaidha na mazingatio. Je! Yupo anaye waidhika? -
وَلَقَدْ جَآءَ ءَالَ فِرْعَوْنَ ٱلنُّذُرُ٤١
Walaqad jaa ala firʿawna alnnuthuru
Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.41
Maelezo
[41] Na watu wa Firauni yaliwajia maonyo ya mfululizo. -
كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذْنَـٰهُمْ أَخْذَ عَزِيزٍ مُّقْتَدِرٍ٤٢
Kaththaboo biayatina kulliha faakhathnahum akhtha ʿazeezin muqtadirin
Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza.42
Maelezo
[42] Walikadhibisha Ishara zetu na miujiza yetu waliyo kuja nayo Mitume wetu. Tukawaangamiza kwa maangamizo ya nguvu yasiyo shindika, ya uwezo mkubwa. -
أَكُفَّارُكُمْ خَيْرٌ مِّنْ أُو۟لَـٰٓئِكُمْ أَمْ لَكُم بَرَآءَةٌ فِى ٱلزُّبُرِ٤٣
Akuffarukum khayrun min olaikum am lakum baraatun fee alzzuburi
Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?43
Maelezo
[43] Ati nyinyi, makafiri, mna nguvu zaidi kuliko hao wa kaumu zilizo tangulia ambao wameangamizwa? Au nyinyi mmetolewa makosani kwa ilivyo teremka katika Vitabu vya mbinguni? -
أَمْ يَقُولُونَ نَحْنُ جَمِيعٌ مُّنتَصِرٌ٤٤
Am yaqooloona nahnu jameeʿun muntasirun
Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.44
Maelezo
[44] Bali ati wanasema hawa makafiri: Sisi ni kikundi kilicho ungana chenye nguvu juu ya maadui wake, hakishindwi. -
سَيُهْزَمُ ٱلْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ ٱلدُّبُرَ٤٥
Sayuhzamu aljamʿu wayuwalloona alddubura
Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.45
Maelezo
[45] Kikundi hicho kitashindwa, na watakimbia mbio wakifurushwa. -
بَلِ ٱلسَّاعَةُ مَوْعِدُهُمْ وَٱلسَّاعَةُ أَدْهَىٰ وَأَمَرُّ٤٦
Bali alssaʿatu mawʿiduhum waalssaʿatu adha waamarru
Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi.46
Maelezo
[46] Bali Kiyama ndio miadi ya adhabu yao. Na Kiyama ni kizito zaidi, na kichungu zaidi. -
إِنَّ ٱلْمُجْرِمِينَ فِى ضَلَـٰلٍ وَسُعُرٍ٤٧
Inna almujrimeena fee dalalin wasuʿurin
Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.47
Maelezo
[47] Hakika wakosefu kutokana na hawa na hao watakuwa katika hilaki na Jahannamu inayo waka moto. -
يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِى ٱلنَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا۟ مَسَّ سَقَرَ٤٨
Yawma yushaboona fee alnnari ʿala wujoohihim thooqoo massa saqara
Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!48
Maelezo
[48] Siku watapo bururwa kifudifudi katika Moto wakiambiwa: Hilikini kwa machungu ya Jahannamu na joto lake! -
إِنَّا كُلَّ شَىْءٍ خَلَقْنَـٰهُ بِقَدَرٍ٤٩
Inna kulla shayin khalaqnahu biqadarin
Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.49
Maelezo
[49] Hakika Sisi tumeumba kila kitu. Tumeviumba kwa kukadiria inavyo hitajia hikima. -
وَمَآ أَمْرُنَآ إِلَّا وَٰحِدَةٌ كَلَمْحٍۭ بِٱلْبَصَرِ٥٠
Wama amruna illa wahidatun kalamhin bialbasari
Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.50
Maelezo
[50] Na haikuwa amri yetu tukitaka kitu ila neno moja tu, nalo ni kusema: "Kuwa", nacho huwa, papo hapo kama kupepesa kwa jicho. -
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَآ أَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ٥١
Walaqad ahlakna ashyaʿakum fahal min muddakirin
Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka?51
Maelezo
[51] Na bila ya shaka Sisi tumekwisha waangamiza wengine walio fanana nanyi katika ukafiri. Je! Yupo aliye waidihika? -
وَكُلُّ شَىْءٍ فَعَلُوهُ فِى ٱلزُّبُرِ٥٢
Wakullu shayin faʿaloohu fee alzzuburi
Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.52
Maelezo
[52] Na kila kitu walicho kifanya duniani kimeandikwa katika madaftari, kimeambatishwa nao. -
وَكُلُّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ مُّسْتَطَرٌ٥٣
Wakullu sagheerin wakabeerin mustatarun
Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.53
Maelezo
[53] Na kila dogo na kubwa katika vitendo limeandikwa. Hakipotei kitu. -
إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَنَهَرٍ٥٤
Inna almuttaqeena fee jannatin wanaharin
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.54
Maelezo
[54] Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani yenye shani kuu, na mito ya namna mbali mbali. -
فِى مَقْعَدِ صِدْقٍ عِندَ مَلِيكٍ مُّقْتَدِرٍۭ٥٥
Fee maqʿadi sidqin ʿinda maleekin muqtadirin
Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.55
Maelezo
[55] Katika baraza ya Haki, hakuna porojo huko wala madhambi, kwa Mwenyewe Mfalme Mtukufu wa uweza
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Qamar maana yake ni nini?
Al-Qamar maana yake ni “Mwezi”.
Surat Al-Qamar iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Qamar iko katika juzuu ya 27.
Surat Al-Qamar ina aya ngapi?
Surat Al-Qamar ina aya 55.
Surat Al-Qamar ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Qamar ni sura ya Makka.
Surat Al-Qamar ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 54 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.