Surat An-Najm (النجم) ni sura ya 53 katika Qur’ani na ina aya 62. Jina lake lina maana ya “Nyota”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 27.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat An-Najm yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat An-Najm kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
وَٱلنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ١
Waalnnajmi itha hawa
Naapa kwa nyota inapo tua!1
Maelezo
[1] Ninaapa kwa nyota inapo tua kwa kuchwa, ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu. -
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ٢
Ma dalla sahibukum wama ghawa
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.2
Maelezo
[2] ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu. -
وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلْهَوَىٰٓ٣
Wama yantiqu ʿani alhawa
Wala hatamki kwa matamanio.3
Maelezo
[3] Wala halitoki katika anayo yatamka ya Qur'ani kwa mapendo ya nafsi yake. -
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْىٌ يُوحَىٰ٤
In huwa illa wahyun yooha
Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; .4
Maelezo
[4] Hii Qur'ani anayo itamka si chochote ila ni Wahyi (Ufunuo) ulio toka kwa Mwenyezi Mungu anamfunulia yeye. -
عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلْقُوَىٰ٥
ʿAllamahu shadeedu alquwa
Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu!5
Maelezo
[5] Aliye mfundisha ufunuo huu ni mwenye nguvu nyingi. -
ذُو مِرَّةٍ فَٱسْتَوَىٰ٦
Thoo mirratin faistawa
Mwenye kutua, akatulia!6
Maelezo
[6] Ambaye ametua akili zake na maoni yake, akasimama sawa sawa katika sura yake; -
وَهُوَ بِٱلْأُفُقِ ٱلْأَعْلَىٰ٧
Wahuwa bialofuqi alaʿla
Naye yuko juu kabisa upeo wa macho.7
Maelezo
[7] Naye yuko upande wa juu katika mbingu upeo wa macho wa mwenye kuangalia. -
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ٨
Thumma dana fatadalla
Kisha akakaribia na akateremka.8
Maelezo
[8] Kisha Jibrili alimkaribia, na akazidi kukaribia, -
فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ٩
Fakana qaba qawsayni aw adna
Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.9
Maelezo
[9] hata akawa ukaribu wake ni kiasi ya mipinde miwili, bali karibu kuliko hivyo. -
فَأَوْحَىٰٓ إِلَىٰ عَبْدِهِۦ مَآ أَوْحَىٰ١٠
Faawha ila ʿabdihi ma awha
Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia.10
Maelezo
[10] Jibrili akamfunulia mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, alicho mfunulia, nao ufunuo huo ni jambo lenye shani kubwa na athari ya mbali kabisa. -
مَا كَذَبَ ٱلْفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ١١
Ma kathaba alfuadu ma raa
Moyo haukusema uwongo uliyo yaona.11
Maelezo
[11] Moyo wa Muhammad haukukanya yale macho yake yaliyo yaona. -
أَفَتُمَـٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ١٢
Afatumaroonahu ʿala ma yara
Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona?12
Maelezo
[12] Hivyo nyinyi mnamkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na mnabishana naye kwa aliyo yaona kwa macho yake? -
وَلَقَدْ رَءَاهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ١٣
Walaqad raahu nazlatan okhra
Na akamwona mara nyingine,13
Maelezo
[13] Na bila ya shaka Muhammad alimwona Jibrili kwa sura yake mara nyengine, -
عِندَ سِدْرَةِ ٱلْمُنتَهَىٰ١٤
ʿInda sidrati almuntaha
Penye Mkunazi wa mwisho.14
Maelezo
[14] Katika pahala pasipo juulikana ila na Mwenyezi Mungu tu, ambapo amepaita Sidratul muntahaa, "Mkunazi wa Mwisho". -
عِندَهَا جَنَّةُ ٱلْمَأْوَىٰٓ١٥
ʿIndaha jannatu almawa
Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa.15
Maelezo
[15] Na akasimulia kuwa hapo ndio ipo Jannatul Ma-awa, Bustani inayo kaliwa. -
إِذْ يَغْشَى ٱلسِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ١٦
Ith yaghsha alssidrata ma yaghsha
Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika.16
Maelezo
[16] Vikafunikwa na kuzibwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, visio weza kuelezwa. -
مَا زَاغَ ٱلْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ١٧
Ma zagha albasaru wama tagha
Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.17
Maelezo
[17] Jicho la Muhammad halikubabaika kwa aliyo yaona, na wala hakukiuka mpaka ya aliyo amrishwa kwa kuona kwake huko. -
لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ ءَايَـٰتِ رَبِّهِ ٱلْكُبْرَىٰٓ١٨
Laqad raa min ayati rabbihi alkubra
Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.18
Maelezo
[18] Hakika ameona mengi katika Ishara za Mwenyezi Mungu na maajabu yake makubwa makubwa. -
أَفَرَءَيْتُمُ ٱللَّـٰتَ وَٱلْعُزَّىٰ١٩
Afaraaytumu allata waalʿuzza
Je! Mmemuona Lata na Uzza?19
Maelezo
[19] Je! Mmeyajua hayo, na mkayafikiri ya kina Lata na Uzza? -
وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلْأُخْرَىٰٓ٢٠
Wamanata alththalithata alokhra
Na Manaat, mwingine wa tatu?20
Maelezo
[20] Na Manata, huyo mwengine wa tatu, mlio wafanya kuwa ni miungu wa kuwaabudu? -
أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلْأُنثَىٰ٢١
Alakumu alththakaru walahu alontha
Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake?21
Maelezo
[21] Mkagawa, nyinyi muwe na watoto wa kiume, na mkamfanyia Mwenyezi Mungu awe na watoto wa kike! -
تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰٓ٢٢
Tilka ithan qismatun deeza
Huo ni mgawanyo wa dhulma!22
Maelezo
[22] Huo basi ni ugawaji wa dhulma, mnamgawia Mwenyezi Mungu kile mnacho kichukia nyinyi wenyewe! -
إِنْ هِىَ إِلَّآ أَسْمَآءٌ سَمَّيْتُمُوهَآ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلْطَـٰنٍ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهْوَى ٱلْأَنفُسُ ۖ وَلَقَدْ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلْهُدَىٰٓ٢٣
In hiya illa asmaon sammaytumooha antum waabaokum ma anzala Allahu biha min sultanin in yattabiʿoona illa alththanna wama tahwa alanfusu walaqad jaahum min rabbihimu alhuda
Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi.23
Maelezo
[23] Hayo masanamu yenu si chochote ila ni majina tu yasiyo na maana yoyote ya kiungu. Mmeyatunga nyinyi na baba zenu kwa kufuata pumbao lenu la upotovu. Mwenyezi Mungu hakuteremsha nayo hoja yoyote ya kusadikisha huo uzushi wenu mnao wadaia. Na hawa hawafuati ila ni dhana tu, na kipendacho nyoyo zao zilio potoka na kuacha maumbile yaliyo sawa. Na hakika yalikwisha wajia kutoka kwa Mola wao Mlezi yenye uwongofu, laiti wangeli ufuata huo! -
أَمْ لِلْإِنسَـٰنِ مَا تَمَنَّىٰ٢٤
Am lilinsani ma tamanna
Ati mtu anakipata kila anacho kitamani?24
Maelezo
[24] Mwanaadamu hapati kila anacho kitamani, ya kupata uombezi wa haya masanamu au mengineyo anayo yatamani kwa nafsi yake. -
فَلِلَّهِ ٱلْـَٔاخِرَةُ وَٱلْأُولَىٰ٢٥
Falillahi alakhiratu waaloola
Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera.25
Maelezo
[25] Kwani mambo yote, ya duniani na Akhera, ni ya Mwenyezi Mungu peke yake. -
۞ وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ لَا تُغْنِى شَفَـٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعْدِ أَن يَأْذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرْضَىٰٓ٢٦
Wakam min malakin fee alssamawati la tughnee shafaʿatuhum shayan illa min baʿdi an yathana Allahu liman yashao wayarda
Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.26
Maelezo
[26] Na malaika wengi wa mbinguni, juu ya ubora wa vyeo vyao, haufai kitu uombezi wao isipo kuwa baada ya kupewa idhini huyo mwombezi na Mwenyewe Mtukufu, na kumridhia huyo mwenye kuombewa. -
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ تَسْمِيَةَ ٱلْأُنثَىٰ٢٧
Inna allatheena la yuminoona bialakhirati layusammoona almalaikata tasmiyata alontha
Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike.27
Maelezo
[27] Hakika hao wasio iamini Akhera ndio bila ya shaka wanao sema kuwa Malaika ni wanawake. Wanasema: Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu! -
وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ ۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغْنِى مِنَ ٱلْحَقِّ شَيْـًٔا٢٨
Wama lahum bihi min ʿilmin in yattabiʿoona illa alththanna wainna alththanna la yughnee mina alhaqqi shayan
Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki.28
Maelezo
[28] Na kwa kauli hii hawana ujuzi wowote. Hawafuati kitu ila dhana zao tu zilio potoka, na dhana haifai kitu mbele ya haki. -
فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا٢٩
Faaʿrid ʿan man tawalla ʿan thikrina walam yurid illa alhayata alddunya
Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia.29
Maelezo
[29] Basi jitenge nao hao makafiri walio ipuuza Qur'ani na ikawa hamu yao si chochote ila uhai wa duniani tu, wakiyakataa yenye maslaha nao. -
ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُم مِّنَ ٱلْعِلْمِ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ ٱهْتَدَىٰ٣٠
Thalika mablaghuhum mina alʿilmi inna rabbaka huwa aʿlamu biman dalla ʿan sabeelihi wahuwa aʿlamu bimani ihtada
Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka.30
Maelezo
[30] Hayo wanayo yafuata katika itikadi zao, na vitendo vyao ndio ukomo walio yafikilia katika ilimu. Hakika Mola wako Mlezi anamjua vyema anaye shikilia upotovu, na anamjua vyema aliye elekea kupokea uwongofu. -
وَلِلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ لِيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ أَسَـٰٓـُٔوا۟ بِمَا عَمِلُوا۟ وَيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ بِٱلْحُسْنَى٣١
Walillahi ma fee alssamawati wama fee alardi liyajziya allatheena asaoo bima ʿamiloo wayajziya allatheena ahsanoo bialhusna
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema.31
Maelezo
[31] Na ni vya Mwenyezi Mungu pekee vyote viliomo katika mbingu na ardhi, kwa kuviumba na kuvidabiri, ili awalipe walio potea wenye kufanya viovu vitendo vyao, na awalipe walio hidika watu wema kwa malipo yaliyo mema. -
ٱلَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَـٰٓئِرَ ٱلْإِثْمِ وَٱلْفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِى بُطُونِ أُمَّهَـٰتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوٓا۟ أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ٣٢
Allatheena yajtaniboona kabaira alithmi waalfawahisha illa allamama inna rabbaka wasiʿu almaghfirati huwa aʿlamu bikum ith anshaakum mina alardi waith antum ajinnatun fee butooni ommahatikum fala tuzakkoo anfusakum huwa aʿlamu bimani ittaqa
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.32
Maelezo
[32] Wema hao ndio wale wanao jitenga na madhambi yenye adhabu kubwa kubwa, na yanayo chukiza mno. Lakini Mwenyezi Mungu husamehe dhambi ndogo ndogo. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkuu wa kughufiria, naye anajua vyema hali zenu. Kwani Yeye ndiye aliye kuumbeni kutokana na ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu katika hali zenu mbali mbali za kukua na kugeuka. Basi msikae mkijisifu nafsi zenu kuwa mmesafika kwa kujigamba na kujifakhari. Na Yeye ndiye Mjuzi mkubwa kabisa wa kila mwenye kumcha na akajisafisha nafsi yake kweli kweli kwa uchamngu wake. -
أَفَرَءَيْتَ ٱلَّذِى تَوَلَّىٰ٣٣
Afaraayta allathee tawalla
Je! Umemwona yule aliye geuka?33
Maelezo
[33] Je! Umezingatia ukamwona anaye puuza kuifuata Haki, -
وَأَعْطَىٰ قَلِيلًا وَأَكْدَىٰٓ٣٤
Waaʿta qaleelan waakda
Na akatoa kidogo, kisha akajizuia?34
Maelezo
[34] Na akatoa kidogo katika mali, na khalafu akakata kabisa kutoa? -
أَعِندَهُۥ عِلْمُ ٱلْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ٣٥
aʿindahu ʿilmu alghaybi fahuwa yara
Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona?35
Maelezo
[35] Je! Huyo anayo ilimu ya kujua mambo ya ghaibu, basi kwa hivyo ndio anayajua yanayo mpelekea kuiacha kuifuata Haki, na akafanya ubakhili wa mali? -
أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِى صُحُفِ مُوسَىٰ٣٦
Am lam yunabba bima fee suhufi moosa
Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa?36
Maelezo
[36] Kwani huyo hakuambiwa yaliomo katika Vitabu vya Musa -
وَإِبْرَٰهِيمَ ٱلَّذِى وَفَّىٰٓ٣٧
Waibraheema allathee waffa
Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi?37
Maelezo
[37] Na Ibrahim, aliye fika ukomo wa kutimiza aliyo agana na Mwenyezi Mungu, -
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ٣٨
Alla taziru waziratun wizra okhra
Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine?38
Maelezo
[38] Ya kwamba hapana mtu ataye mbebea dhambi mwenginewe? -
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَـٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ٣٩
Waan laysa lilinsani illa ma saʿa
Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe?39
Maelezo
[39] Na kwamba mtu hapati ila malipo ya vitendo vyake mwenyewe. -
وَأَنَّ سَعْيَهُۥ سَوْفَ يُرَىٰ٤٠
Waanna saʿyahu sawfa yura
Na kwamba vitendo vyake vitaonekana?40
Maelezo
[40] Na kwamba vitendo vyake vitakuja tangazwa, na ataviona Siku ya Kiyama, iwe ni kumtukuza mtenda mema, na kumkebehi mtenda maovu. -
ثُمَّ يُجْزَىٰهُ ٱلْجَزَآءَ ٱلْأَوْفَىٰ٤١
Thumma yujzahu aljazaa alawfa
Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu.41
Maelezo
[41] Kisha kila mtu atalipwa malipo anayo stahiki. -
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلْمُنتَهَىٰ٤٢
Waanna ila rabbika almuntaha
Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho.42
Maelezo
[42] Na kwamba kwa hakika ni kwa Mola wako Mlezi, wala si kwa mwenginewe, ndio miadi ya kurejea. -
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ٤٣
Waannahu huwa adhaka waabka
Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio.43
Maelezo
[43] Na Yeye peke yake ni Mwenye uweza wa kuufanya uso uonyeshe furaha au maudhiko, na pia ni Mwenye kuziumba sababu za starehe na dhiki. -
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا٤٤
Waannahu huwa amata waahya
Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha.44
Maelezo
[44] Na hakika ni Yeye, ndiye Mwenye kuondoa uhai, na kuuleta. -
وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوْجَيْنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰ٤٥
Waannahu khalaqa alzzawjayni alththakara waalontha
Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike45
Maelezo
[45] Na Yeye ndiye aliye umba vitu kwa jozi, yaani dume na jike, binaadamu na wanyama, -
مِن نُّطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ٤٦
Min nutfatin itha tumna
Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa.46
Maelezo
[46] Kutokana na manii yanayo miminwa. Makusudio ya Aya hii tukufu ni kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba Yeye ameumba waume na wake katika wanaadamu na wanyama wote kutokana na tone ya manii ambayo humo humo mna ume na uke. Na juu ya udogo wake na udhaifu wake ndio chemchem ya uhai. Umuujiza wa Qur'ani unadhihirika katika Aya hii tukufu ukikumbuka kuwa ulimwengu ulikuwa haujui mpaka hivi karibu kuwa katika maji ya mwanamume ndio zimo mbegu "sperms" na katika maji ya mwanamke mna vijiyai "ova", ndio vikikutana vijidudu vya manii ya mwanamume na vijiyai vya mwanamke vikawa kitu kimoja ndio hiyo huwa mimba. Ukweli huu ulitajwa na Qur'ani kabla ya kuvumbuliwa na ilimu za Sayansi. -
وَأَنَّ عَلَيْهِ ٱلنَّشْأَةَ ٱلْأُخْرَىٰ٤٧
Waanna ʿalayhi alnnashata alokhra
Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine.47
Maelezo
[47] Na juu yake Yeye ndio kufufua baada ya kifo. -
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغْنَىٰ وَأَقْنَىٰ٤٨
Waannahu huwa aghna waaqna
Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha.48
Maelezo
[48] Na Yeye ndiye anaye toa kinacho tosheleza, na akaridhisha kwa kinacho kinaisha na cha kuweka akiba. -
وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعْرَىٰ٤٩
Waannahu huwa rabbu alshshiʿra
Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra.49
Maelezo
[49] Na hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa hii nyota kubwa inayo itwa Shii'ra (Sirius, Dog Star). Makusudio hapa ni Nyota hiyo inayo itwa Ash-shi'ra Alyamaaniya, au wanavyo ita Wazungu Sirius au Dog Star. Nyota hii inang'ara kwa nguvu zaidi kuliko nyota zote ziliomo katika kikundi cha nyota kinacho itwa Alkalbu l-akbar, kwa Kizungu Canis Major au Greater Dog. Nyota hiyo ndiyo inayo zagaa sana mbinguni, na huonekana kusini ya mstari wa kati wa mbinguni kiasi ya daraja 18. Na kwa jina hilo la Nyota ya Mbwa ikijuulikana hata miaka elfu tatu ilio pita. Katika mabaki ya michoro ya Mafirauni wa Misri imeashiriwa pia. Mwenyezi Mungu ameitaja khasa kwa kuwa Waarabu walikuwa wakiiabudu hapo kale, na pia Wamisri wa zamani, kwani kutokea kwake upande wa mashariki katikati ya mwezi wa Julai kabla ya kuchomoza jua kulikuwa kunawafikiana na wakati wa mafuriko ya Misri ya kati, yaani katika tukio muhimu kabisa katika ulimwengu huo wa kale. Na tukio hili huenda ndilo lilio fanya kuanzisha kuwekea kiwango urefu wa mwaka katika dunia nzima. Kwani kudhihiri Nyota ya Shiira kabla ya kuchomoza jua hakutokei ila mara moja tu katika mwaka. Basi huu ndio mwanzo wa mwaka mpya. -
وَأَنَّهُۥٓ أَهْلَكَ عَادًا ٱلْأُولَىٰ٥٠
Waannahu ahlaka ʿadan aloola
Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza,50
Maelezo
[50] Na Yeye ndiye aliye wateketeza kina A'di wa mwanzo, kaumu ya Nabii Hudi. Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha. -
وَثَمُودَا۟ فَمَآ أَبْقَىٰ٥١
Wathamooda fama abqa
Na Thamudi hakuwabakisha,51
Maelezo
[51] Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha. -
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَىٰ٥٢
Waqawma noohin min qablu innahum kanoo hum athlama waatgha
Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi;52
Maelezo
[52] Na aliwaangamiza kaumu ya Nuhu kabla ya kuwaangamiza A'di na Thamudi. Hakika hao walikuwa wamekithiri kudhulumu, na wamezidi kwa uasi kuliko A'di na Thamudi. -
وَٱلْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ٥٣
Waalmutafikata ahwa
Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua.53
Maelezo
[53] Na miji ya kaumu Lut'i iliyo pinduliwa juu chini, ni Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliye ipindua. -
فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ٥٤
Faghashshaha ma ghashsha
Vikaifunika vilivyo funika.54
Maelezo
[54] Akaizunguka kwa kuiadhibu kama alivyo izunguka. -
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ٥٥
Fabiayyi alai rabbika tatamara
Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka?55
Maelezo
[55] Basi katika neema za Mola wako Mlezi una shaka nayo ipi? -
هَـٰذَا نَذِيرٌ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلْأُولَىٰٓ٥٦
Hatha natheerun mina alnnuthuri aloola
Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani.56
Maelezo
[56] Hii Qur'ani ni onyo katika jinsi ya yale yale maonyo ya kale waliyo onywa kwayo watu walio tangulia. -
أَزِفَتِ ٱلْـَٔازِفَةُ٥٧
Azifati alazifatu
Kiyama kimekaribia!57
Maelezo
[57] Kiyama kimekaribia; -
لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ٥٨
Laysa laha min dooni Allahi kashifatun
Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu.58
Maelezo
[58] Na wala hapana wa kuujuulisha wakati kitapo tokea ila mwenyewe Mwenyezi Mungu. -
أَفَمِنْ هَـٰذَا ٱلْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ٥٩
Afamin hatha alhadeethi taʿjaboona
Je! Mnayastaajabia maneno haya?59
Maelezo
[59] Hivyo nyinyi mnapinga kila la kweli? Na mnaistaajabia kwa kuikaataa hii Qur'ani? -
وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ٦٠
Watadhakoona wala tabkoona
Na mnacheka, wala hamlii?60
Maelezo
[60] Na mnacheka kwa kejeli na maskhaara, wala hamlii kama wafanyavyo wenye yakini, -
وَأَنتُمْ سَـٰمِدُونَ٦١
Waantum samidoona
Nanyi mmeghafilika?61
Maelezo
[61] Nanyi mmo katika pumbao na kutakabari? -
فَٱسْجُدُوا۟ لِلَّهِ وَٱعْبُدُوا۟ ۩٦٢
Faosjudoo lillahi waoʿbudoo
Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.62
Maelezo
[62] Basi msujudieni Mwenyezi Mungu aliye iteremsha Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu wote, na muabuduni Yeye tu peke yake Mwenye kutukuka kwa utukufu wake.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat An-Najm maana yake ni nini?
An-Najm maana yake ni “Nyota”.
Surat An-Najm iko katika juzuu ya ngapi?
Surat An-Najm iko katika juzuu ya 27.
Surat An-Najm ina aya ngapi?
Surat An-Najm ina aya 62.
Surat An-Najm ni ya Makka au ya Madina?
Surat An-Najm ni sura ya Makka.
Surat An-Najm ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 53 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.