سورة الجن

Surat Al-Jinn kwa Kiswahili

Majini

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Jinn (الجن) ni sura ya 72 katika Qur’ani na ina aya 28. Jina lake lina maana ya “Majini”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 29.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Jinn yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Jinn kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. قُلْ أُوحِىَ إِلَىَّ أَنَّهُ ٱسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ ٱلْجِنِّ فَقَالُوٓا۟ إِنَّا سَمِعْنَا قُرْءَانًا عَجَبًا۝١

    Qul oohiya ilayya annahu istamaʿa nafarun mina aljinni faqaloo inna samiʿna quranan ʿajaban

    Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!1

    Maelezo
    [1] Ewe Muhammad! Waambie watu wako: Nimepata wahyi kwamba kikundi cha majini kimesikia kusoma kwangu Qur'ani, nao wakawaambia wenzao: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya namna ya peke yake, hatujapata kusikia mfano wake kabla yake,
  2. يَهْدِىٓ إِلَى ٱلرُّشْدِ فَـَٔامَنَّا بِهِۦ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَآ أَحَدًا۝٢

    Yahdee ila alrrushdi faamanna bihi walan nushrika birabbina ahadan

    Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi.2

    Maelezo
    [2] inaitia kwenye uwongofu na usawa. Kwa hivyo tumeiamini hiyo Qur'ani tuliyo isikia; na kabisa hatutamshirikisha Mola wetu Mlezi aliye tuumba na kutulea na chochote katika waja wake.
  3. وَأَنَّهُۥ تَعَـٰلَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا ٱتَّخَذَ صَـٰحِبَةً وَلَا وَلَدًا۝٣

    Waannahu taʿala jaddu rabbina ma ittakhatha sahibatan wala waladan

    Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hana mke wala mwana.3

    Maelezo
    [3] Na kwamba hakika cheo na utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka; hana mke wala mwana.
  4. وَأَنَّهُۥ كَانَ يَقُولُ سَفِيهُنَا عَلَى ٱللَّهِ شَطَطًا۝٤

    Waannahu kana yaqoolu safeehuna ʿala Allahi shatatan

    Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongo ulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.4

    Maelezo
    [4] Na hakika wajinga katika sisi walikuwa wakimzulia Mwenyezi Mungu maneno yaliyo kuwa mbali kabisa na ukweli na kuwa sawa.
  5. وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن تَقُولَ ٱلْإِنسُ وَٱلْجِنُّ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا۝٥

    Waanna thananna an lan taqoola alinsu waaljinnu ʿala Allahi kathiban

    Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo Mwenyezi Mungu.5

    Maelezo
    [5] Na hakika sisi tulikuwa tunadhani kuwa haiwi binaadamu au jini kumzulia Mwenyezi Mungu jambo ambalo si laiki naye kusifika nalo.
  6. وَأَنَّهُۥ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ ٱلْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ ٱلْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا۝٦

    Waannahu kana rijalun mina alinsi yaʿoothoona birijalin mina aljinni fazadoohum rahaqan

    Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafuta kujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.6

    Maelezo
    [6] Na walikuwako wanaume katika wanaadamu wakitafuta ulinzi kwa wanaume wa kijini. Basi hao binaadamu hawakuwazidishia majini ila kuzidi uasi na ujinga na ujeuri.
  7. وَأَنَّهُمْ ظَنُّوا۟ كَمَا ظَنَنتُمْ أَن لَّن يَبْعَثَ ٱللَّهُ أَحَدًا۝٧

    Waannahum thannoo kama thanantum an lan yabʿatha Allahu ahadan

    Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwa Mwenyezi Mungu hatamleta Mtume.7

    Maelezo
    [7] Na hakika majini walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, enyi binaadamu, kwamba Mwenyezi Mungu hatamfufua yeyote baada ya kwisha kufa, wala hatowaletea watu Mtume yeyote wa kibinaadamu.
  8. وَأَنَّا لَمَسْنَا ٱلسَّمَآءَ فَوَجَدْنَـٰهَا مُلِئَتْ حَرَسًا شَدِيدًا وَشُهُبًا۝٨

    Waanna lamasna alssamaa fawajadnaha muliat harasan shadeedan washuhuban

    Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na vimondo.8

    Maelezo
    [8] Na hakika sisi tulitaka kufikilia mbinguni, tukakuta kumejaa walinzi wa kimalaika wenye nguvu, na vimondo vinavyo unguza kutoka upande huo.
  9. وَأَنَّا كُنَّا نَقْعُدُ مِنْهَا مَقَـٰعِدَ لِلسَّمْعِ ۖ فَمَن يَسْتَمِعِ ٱلْـَٔانَ يَجِدْ لَهُۥ شِهَابًا رَّصَدًا۝٩

    Waanna kunna naqʿudu minha maqaʿida lilssamʿi faman yastamiʿi alana yajid lahu shihaban rasadan

    Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza; lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!9

    Maelezo
    [9] Na sisi kabla ya leo tulikuwa tukikaa pande za mbinguni kwenye makao kwa ajili ya kuchunguza khabari za mbinguni. Lakini sasa mwenye kutaka kusikiliza anakuta vimondo vinamngojea kumzuia na kumteketeza.
  10. وَأَنَّا لَا نَدْرِىٓ أَشَرٌّ أُرِيدَ بِمَن فِى ٱلْأَرْضِ أَمْ أَرَادَ بِهِمْ رَبُّهُمْ رَشَدًا۝١٠

    Waanna la nadree asharrun oreeda biman fee alardi am arada bihim rabbuhum rashadan

    Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanao kaa kwenye ardhi au Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu.10

    Maelezo
    [10] Na hakika sisi hatujui imekusudiwa adhabu kwa walioko katika ardhi kwa huku kulindwa mbingu hata ikazuiliwa kusikilizwa, au Mola wao Mlezi anawatakia kheri na uwongofu?
  11. وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّـٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ كُنَّا طَرَآئِقَ قِدَدًا۝١١

    Waanna minna alssalihoona waminna doona thalika kunna taraiqa qidadan

    Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyume na hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.11

    Maelezo
    [11] Na hakika miongoni mwetu wapo walio wema wachamngu, na miongoni mwetu pia wapo walio kinyume na hivyo. Na hao ni walio wastani katika wema wao. Kwa hivyo sisi ni wa makundi mbali mbali.
  12. وَأَنَّا ظَنَنَّآ أَن لَّن نُّعْجِزَ ٱللَّهَ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَن نُّعْجِزَهُۥ هَرَبًا۝١٢

    Wanna thananna an lan nuʿjiza Allaha fee alardi walan nuʿjizahu haraban

    Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, wala hatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.12

    Maelezo
    [12] Na hakika sisi tumeyakinika kwamba hatutamshinda Mwenyezi Mungu popote tutapo kuwapo katika ardhi, wala hatutamshinda hata tukifanya tuikimbie hukumu yake kwendea mbinguni.
  13. وَأَنَّا لَمَّا سَمِعْنَا ٱلْهُدَىٰٓ ءَامَنَّا بِهِۦ ۖ فَمَن يُؤْمِنۢ بِرَبِّهِۦ فَلَا يَخَافُ بَخْسًا وَلَا رَهَقًا۝١٣

    Waanna lamma samiʿna alhuda amanna bihi faman yumin birabbihi fala yakhafu bakhsan wala rahaqan

    Nasi tulipo usikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.13

    Maelezo
    [13] Na hakika sisi tulipo isikia Qur'ani tuliiamini. Na mwenye kumuamini Mola wake Mlezi basi hachelei kupunguziwa chochote katika mema yake, wala kudhulumiwa kwa kuzidishiwa maovu yake.
  14. وَأَنَّا مِنَّا ٱلْمُسْلِمُونَ وَمِنَّا ٱلْقَـٰسِطُونَ ۖ فَمَنْ أَسْلَمَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ تَحَرَّوْا۟ رَشَدًا۝١٤

    Waanna minna almuslimoona waminna alqasitoona faman aslama faolaika taharraw rashadan

    Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanao acha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu.14

    Maelezo
    [14] Na hakika kati yetu wapo Waislamu wenye kuikubali Haki, na miongoni mwetu wapo wenye kuiacha njia ya uwongofu. Basi wenye kusilimu hao wameifuata njia ya Haki, na ni wenye kufanya jitihada katika kuikhiari njia hiyo.
  15. وَأَمَّا ٱلْقَـٰسِطُونَ فَكَانُوا۟ لِجَهَنَّمَ حَطَبًا۝١٥

    Waama alqasitoona fakanoo lijahannama hataban

    Na ama wanao acha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu.15

    Maelezo
    [15] Ama majeuri walio iacha njia ya Uislamu basi hao watakuwa ndio kuni za Jahannamu.
  16. وَأَلَّوِ ٱسْتَقَـٰمُوا۟ عَلَى ٱلطَّرِيقَةِ لَأَسْقَيْنَـٰهُم مَّآءً غَدَقًا۝١٦

    Waallawi istaqamoo ʿala alttareeqati laasqaynahum maan ghadaqan

    Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanywesha maji kwa wingi,16

    Maelezo
    [16] Na hakika lau kuwa watu na majini wakifuata Njia ya Uislamu, wala wasende upogo wakaiwacha, basi bila ya shaka tutawanywesha maji mengi yatakayo enea nyakati za haja.
  17. لِّنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَمَن يُعْرِضْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِۦ يَسْلُكْهُ عَذَابًا صَعَدًا۝١٧

    Linaftinahum feehi waman yuʿrid ʿan thikri rabbihi yaslukhu ʿathaban saʿadan

    Ili tuwajaribu kwa hayo. Na anaye puuza kumkumbuka Mola wake Mlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu.17

    Maelezo
    [17] Ili tuwajaribu tuwaone vipi watavyo mshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema anazo waneemesha. Na mwenye kukengeuka na ibada ya Mola wake Mlezi atamtia katika adhabu ya mashaka asiyo yaweza kuyachukua.
  18. وَأَنَّ ٱلْمَسَـٰجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدْعُوا۟ مَعَ ٱللَّهِ أَحَدًا۝١٨

    Waanna almasajida lillahi fala tadʿoo maʿa Allahi ahadan

    Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.18

    Maelezo
    [18] Na imefunuliwa kwangu kwamba kwa hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu peke yake. Basi msimuabudu yeyote pamoja na Mwenyezi Mungu.
  19. وَأَنَّهُۥ لَمَّا قَامَ عَبْدُ ٱللَّهِ يَدْعُوهُ كَادُوا۟ يَكُونُونَ عَلَيْهِ لِبَدًا۝١٩

    Waannahu lamma qama ʿabdu Allahi yadʿoohu kadoo yakoonoona ʿalayhi libadan

    Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu alipo simama kumwomba, wao walikuwa karibu kumzonga!19

    Maelezo
    [19] Na imefunuliwa kwangu kwamba alipo simama Mja wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, katika Swala yake akimuabudu Mwenyezi Mungu, majini walijikusanya makundi kwa makundi, wakistaajabu kwa waliyo kuwa wakiyaona na wakiyasikia.
  20. قُلْ إِنَّمَآ أَدْعُوا۟ رَبِّى وَلَآ أُشْرِكُ بِهِۦٓ أَحَدًا۝٢٠

    Qul innama adʿoo rabbee wala oshriku bihi ahadan

    Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishi Yeye na yeyote.20

    Maelezo
    [20] Sema: Hakika mimi namuabudu Mola wangu Mlezi peke yake, wala simshirikishi na yeyote katika ibada.
  21. قُلْ إِنِّى لَآ أَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا رَشَدًا۝٢١

    Qul innee la amliku lakum darran wala rashadan

    Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni.21

    Maelezo
    [21] Sema: Mimi sina uweza wowote juu yenu wa kukuondoleeni madhara, wala kukuleteeni uwongofu na manufaa.
  22. قُلْ إِنِّى لَن يُجِيرَنِى مِنَ ٱللَّهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلْتَحَدًا۝٢٢

    Qul innee lan yujeeranee mina Allahi ahadun walan ajida min doonihi multahadan

    Sema: Hakika hapana yeyote awezae kunilinda na Mwenyezi Mungu, wala sitapata pa kukimbilia isipo kuwa kwake Yeye tu.22

    Maelezo
    [22] Sema: Hakika mimi hapana yeyote awezae kuniondolea adhabu nikimuasi Mwenyezi Mungu. Wala sipati pa kukimbilia, kuikimbia adhabu yake.
  23. إِلَّا بَلَـٰغًا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِسَـٰلَـٰتِهِۦ ۚ وَمَن يَعْصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا۝٢٣

    Illa balaghan mina Allahi warisalatihi waman yaʿsi Allaha warasoolahu fainna lahu nara jahannama khalideena feeha abadan

    Ila nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake. Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele.23

    Maelezo
    [23] Lakini niliwezalo ni kufikisha Ujumbe wa Mwenyezi Mungu na Risala zake alizo nituma nizifikishe. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipuuza Dini ya Mwenyezi Mungu, basi hakika mtu huyo atapata Moto wa Jahannamu abakie humo milele.
  24. حَتَّىٰٓ إِذَا رَأَوْا۟ مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ أَضْعَفُ نَاصِرًا وَأَقَلُّ عَدَدًا۝٢٤

    Hatta itha raaw ma yooʿadoona fasayaʿlamoona man adʿafu nasiran waaqallu ʿadadan

    Hata watakapo yaona wanayo ahidiwa, ndipo watakapo jua ni nani mwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.24

    Maelezo
    [24] Hata watakapo iona adhabu waliyo ahidiwaa, hapo basi watajua wakati itapo shuka, nani mwenye msaidizi dhaifu asiye na nguvu, na yupi mchache wa idadi. Ni wao au Waumini?
  25. قُلْ إِنْ أَدْرِىٓ أَقَرِيبٌ مَّا تُوعَدُونَ أَمْ يَجْعَلُ لَهُۥ رَبِّىٓ أَمَدًا۝٢٥

    Qul in adree aqareebun ma tooʿadoona am yajʿalu lahu rabbee amadan

    Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayo ahidiwa, au Mola wangu Mlezi atayawekea muda mrefu.25

    Maelezo
    [25] Sema: Enyi makafiri! Sijui ni karibu hiyo adhabu mliyo ahidiwa, au Mola wangu Mlezi ataifanya iwe mbali?
  26. عَـٰلِمُ ٱلْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَىٰ غَيْبِهِۦٓ أَحَدًا۝٢٦

    ʿalimu alghaybi fala yuthhiru ʿala ghaybihi ahadan

    Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake,26

    Maelezo
    [26] Yeye ndiye Mjuzi wa ghaibu, yaliyo siri. Hapana mmoja katika viumbe vyake anaye ijua siri yake,
  27. إِلَّا مَنِ ٱرْتَضَىٰ مِن رَّسُولٍ فَإِنَّهُۥ يَسْلُكُ مِنۢ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِۦ رَصَدًا۝٢٧

    Illa mani irtada min rasoolin fainnahu yasluku min bayni yadayhi wamin khalfihi rasadan

    Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzi mbele yake na nyuma yake.27

    Maelezo
    [27] ila Mtume aliye mridhia kumjuvya baadhi ya hiyo siri. Naye humwekea mbele ya huyo Mtume na nyuma yake Malaika wa kumkinga na wasiwasi.
  28. لِّيَعْلَمَ أَن قَدْ أَبْلَغُوا۟ رِسَـٰلَـٰتِ رَبِّهِمْ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيْهِمْ وَأَحْصَىٰ كُلَّ شَىْءٍ عَدَدًۢا۝٢٨

    Liyaʿlama an qad ablaghoo risalati rabbihim waahata bima ladayhim waahsa kulla shayin ʿadadan

    Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi, na Yeye anayajua vyema yote walio nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu.28

    Maelezo
    [28] Ili Mwenyezi Mungu ayajue hayo yametokea kwa kuwafikiana na alivyo kadiria, ya kwamba Manabii hakika wamefikisha Risala za Mola wao Mlezi. Na kwa hakika Yeye kesha jua kwa kufananua yote waliyo nayo, na anajua idadi ya viumbe vyote. Hapana kitu kinacho mpotea Yeye.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Jinn maana yake ni nini?

Al-Jinn maana yake ni “Majini”.

Surat Al-Jinn iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Jinn iko katika juzuu ya 29.

Surat Al-Jinn ina aya ngapi?

Surat Al-Jinn ina aya 28.

Surat Al-Jinn ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Jinn ni sura ya Makka.

Surat Al-Jinn ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 72 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.