Surat Nuh (نوح) ni sura ya 71 katika Qur’ani na ina aya 28. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 29.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Nuh yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Nuh kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
إِنَّآ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِۦٓ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ١
Inna arsalna noohan ila qawmihi an anthir qawmaka min qabli an yatiyahum ʿathabun aleemun
Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.1
Maelezo
[1] Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake, na tukamwambia: Waonye watu wako kabla haijawajia adhabu yenye machungu makali. -
قَالَ يَـٰقَوْمِ إِنِّى لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ٢
Qala ya qawmi innee lakum natheerun mubeenun
Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu!2
Maelezo
[2] Nuh'u akasema: Enyi watu wangu! Hakika mimi ni mwonyaji kwenu, nina risala kutoka kwa Mola wenu Mlezi kwa lugha mnayo ijua, -
أَنِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ٣
Ani oʿbudoo Allaha waittaqoohu waateeʿooni
Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii.3
Maelezo
[3] Ya kwamba mumt'ii Mwenyezi Mungu, na mumnyenyekee katika kutimiza waajibu zote; na mwogopeni Yeye kwa kuacha mnayo katazwa, na nit'iini mimi katika ninayo kunasihini. -
يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ إِذَا جَآءَ لَا يُؤَخَّرُ ۖ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ٤
Yaghfir lakum min thunoobikum wayuakhkhirkum ila ajalin musamman inna ajala Allahi itha jaa la yuakhkharu law kuntum taʿlamoona
Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua!4
Maelezo
[4] Ndipo Mwenyezi Mungu atapo kusameheni madhambi yenu, na atakupeni umri mrefu mpaka ifike ajali iliyo wekwa mwisho wa umri wenu. Hakika mauti yakija hayaakhirishwi kabisa! Lau kuwa mngeli jua majuto mtakayo kuwa nayo utapo kwisha muda wenu mngeli amini. -
قَالَ رَبِّ إِنِّى دَعَوْتُ قَوْمِى لَيْلًا وَنَهَارًا٥
Qala rabbi innee daʿawtu qawmee laylan wanaharan
Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana!5
Maelezo
[5] Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu waamini usiku na mchana bila ya kuchoka, -
فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَآءِىٓ إِلَّا فِرَارًا٦
Falam yazidhum duʿaee illa firaran
Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia.6
Maelezo
[6] Hawakuzidishwa na wito wangu ila kuukimbia ut'iifu wako. -
وَإِنِّى كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوٓا۟ أَصَـٰبِعَهُمْ فِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَٱسْتَغْشَوْا۟ ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا۟ وَٱسْتَكْبَرُوا۟ ٱسْتِكْبَارًا٧
Wainnee kullama daʿawtuhum litaghfira lahum jaʿaloo asabiʿahum fee athanihim waistaghshaw thiyabahum waasarroo waistakbaroo istikbaran
Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!7
Maelezo
[7] Na mimi kila nikiwataka wakuamini Wewe upate kuwasamehe, hubandika vidole vyao kwenye masikio yao ili wasisikie wito wangu, na hujifunika kwa maguo yao ili wasiuone uso wangu! Na wakasimama kidete juu ya ukafiri wao, na wakatakabari kutakabari kukubwa mno! -
ثُمَّ إِنِّى دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا٨
Thumma innee daʿawtuhum jiharan
Tena niliwaita kwa uwazi!8
Maelezo
[8] Kisha nikawaita waje kwako kwa sauti ya juu, -
ثُمَّ إِنِّىٓ أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا٩
Thumma innee aʿlantu lahum waasrartu lahum israran
Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri.9
Maelezo
[9] kisha nikaudhihirisha wito kwa namna moja, na nikawaita kisirisiri kwa namna nyengine, ili nijaribu kila njia. -
فَقُلْتُ ٱسْتَغْفِرُوا۟ رَبَّكُمْ إِنَّهُۥ كَانَ غَفَّارًا١٠
Faqultu istaghfiroo rabbakum innahu kana ghaffaran
Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.10
Maelezo
[10] Nikawambia watu wangu: Takeni kwa Mola wenu Mlezi maghfira kwa kufru zenu na maasi yenu. Kwani Yeye bado ni Mwingi wa kusamehe madhambi ya mwenye kurejea kwake. -
يُرْسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا١١
Yursili alssamaa ʿalaykum midraran
Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.11
Maelezo
[11] Atakuleteeni mawingu yatakayo miminika mvua kwa wingi, -
وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَٰلٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّـٰتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَـٰرًا١٢
Wayumdidkum biamwalin wabaneena wayajʿal lakum jannatin wayajʿal lakum anharan
Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito.12
Maelezo
[12] Na atakupeni mali na wana, na hayo ndiyo mapambo ya dunia, na atakupeni mashamba mtayo starehea kwa uzuri wake na matunda yake, na atakujaalieni mito ya kunyweshea mazao yenu na mifugo yenu. -
مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّهِ وَقَارًا١٣
Ma lakum la tarjoona lillahi waqaran
Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu?13
Maelezo
[13] Mna nini nyinyi hata hamumtukuzi Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kutukuzwa, ili mtaraji akukirimuni kwa kukuokoeni na adhabu, -
وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا١٤
Waqad khalaqakum atwaran
Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?14
Maelezo
[14] Na hali Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa madaraja, tangu tone ya manii, kisha pande la damu, kisha pande la nyama, kisha mafupa na nyama? -
أَلَمْ تَرَوْا۟ كَيْفَ خَلَقَ ٱللَّهُ سَبْعَ سَمَـٰوَٰتٍ طِبَاقًا١٥
Alam taraw kayfa khalaqa Allahu sabʿa samawatin tibaqan
Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?15
Maelezo
[15] Kwani huoni vipi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba, moja juu ya moja, -
وَجَعَلَ ٱلْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ ٱلشَّمْسَ سِرَاجًا١٦
Wajaʿala alqamara feehinna nooran wajaʿala alshshamsa sirajan
Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?16
Maelezo
[16] Na akaufanya mwezi katika mbingu hizo unatoa nuru, na akalifanya jua ni taa ambayo kwayo watu wa duniani ndio wanaona kwa mwangaza wake yote wanayo hitajia kuyaona? -
وَٱللَّهُ أَنۢبَتَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ نَبَاتًا١٧
WaAllahu anbatakum mina alardi nabatan
Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea.17
Maelezo
[17] Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na ardhi, akakuotesheni kama miema kwa njia ya ajabu, -
ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا١٨
Thumma yuʿeedukum feeha wayukhrijukum ikhrajan
Kisha atakurudsheni humo na atakutoeni tena.18
Maelezo
[18] Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na ardhi, akakuotesheni kama miema kwa njia ya ajabu, kisha baada ya kufa atakurejesheni huko huko kwenye ardhi, na tena atakutoeni huko kwa hakika hapana hivi wala hivi. -
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ بِسَاطًا١٩
WaAllahu jaʿala lakumu alarda bisatan
Na Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati.19
Maelezo
[19] Na Mwenyezi Mungu ameifanya ardhi iliyo kunjuliwa ili mpate kwenda humo katika njia zenye wasaa. -
لِّتَسْلُكُوا۟ مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا٢٠
Litaslukoo minha subulan fijajan
Ili mtembee humo katika njia zilizo pana.20
Maelezo
[20] Na Mwenyezi Mungu ameifanya ardhi iliyo kunjuliwa ili mpate kwenda humo katika njia zenye wasaa. -
قَالَ نُوحٌ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِى وَٱتَّبَعُوا۟ مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُۥ وَوَلَدُهُۥٓ إِلَّا خَسَارًا٢١
Qala noohun rabbi innahum ʿasawnee waittabaʿoo man lam yazidhu maluhu wawaladuhu illa khasaran
Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara.21
Maelezo
[21] Alisema Nuh'u: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikatalia mimi niliyo waamrisha ya kuamini na kutaka msamaha, na wakawafuata madhaifu miongoni mwao ambao mali yao na watoto wao hawawazidishii ila khasara tupu katika Akhera. -
وَمَكَرُوا۟ مَكْرًا كُبَّارًا٢٢
Wamakaroo makran kubbaran
Na wakapanga vitimbi vikubwa.22
Maelezo
[22] Na vitimbi vya hao wenye mali mengi, na wana wengi, kwa wanyonge wanao wafuata ni vitimbi vilivyo fika ukomo kwa ukubwa. -
وَقَالُوا۟ لَا تَذَرُنَّ ءَالِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا٢٣
Waqaloo la tatharunna alihatakum wala tatharunna waddan wala suwaʿan wala yaghootha wayaʿooqa wanasran
Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra.23
Maelezo
[23] Na wao wakiwaambia: Msiache kuiabudu miungu yenu, wala msimwache Wadda, wala Suwaa' , wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra. Na hawa walikuwa miungu ya masanamu iliyo chongwa kwa sura ya wanyama namna mbali mbali. -
وَقَدْ أَضَلُّوا۟ كَثِيرًا ۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا ضَلَـٰلًا٢٤
Waqad adalloo katheeran wala tazidi alththalimeena illa dalalan
Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.24
Maelezo
[24] Na miungu hii iliwapoteza watu wengi. Na wala huwazidishii wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na inda, ili kuzidi kubaidika na Haki. -
مِّمَّا خَطِيٓـَٔـٰتِهِمْ أُغْرِقُوا۟ فَأُدْخِلُوا۟ نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا۟ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ أَنصَارًا٢٥
Mimma khateeatihim oghriqoo faodkhiloo naran falam yajidoo lahum min dooni Allahi ansaran
Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.25
Maelezo
[25] Kwa sababu ya madhambi yao wakazamishwa kwa tofani, na baada ya kuangamizwa kwao wakatiwa Motoni kwenye moto mkali wa kuwaka na kuteketeza, na wala wasipate yeyote baada ya kumkosa Mwenyezi Mungu, wa kuwanusuru na kuwakinga na adhabu! -
وَقَالَ نُوحٌ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى ٱلْأَرْضِ مِنَ ٱلْكَـٰفِرِينَ دَيَّارًا٢٦
Waqala noohun rabbi la tathar ʿala alardi mina alkafireena dayyaran
Na Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!26
Maelezo
[26] Na Nuh'u akasema baada ya kukata tamaa nao watu wake: Mola wangu Mlezi! Usimwache yeyote katika hao wanao kukataa Wewe akabaki akizunguka juu ya ardhi! -
إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا۟ عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوٓا۟ إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا٢٧
Innaka in tatharhum yudilloo ʿibadaka wala yalidoo illa fajiran kaffaran
Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.27
Maelezo
[27] Ewe Mola wangu Mlezi! Ukiwaacha hao bila ya kuwateketeza na kuwang'oa watawatia waja wako katika upotovu, na wao hawatozaa ila wenye kupotoka vile vile wakaiacha haki, na wakakithiri kukukanya na kukuasi. -
رَّبِّ ٱغْفِرْ لِى وَلِوَٰلِدَىَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِىَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا تَبَارًۢا٢٨
Rabbi ighfir lee waliwalidayya waliman dakhala baytiya muminan walilmumineena waalmuminati wala tazidi alththalimeena illa tabaran
Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.28
Maelezo
[28] Mola wangu Mlezi! Nisamehe mimi na wazazi wangu ambao ndio walio kuwa ni sababu ya kuzaliwa mimi, na kila mwenye kuingia nyumbani kwangu kwa kukuamini Wewe, na uwasamehe Waumini wote wanaume na wanawake. Na usiwazidishie makafiri ila kuwaangamiza.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Nuh iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Nuh iko katika juzuu ya 29.
Surat Nuh ina aya ngapi?
Surat Nuh ina aya 28.
Surat Nuh ni ya Makka au ya Madina?
Surat Nuh ni sura ya Makka.
Surat Nuh ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 71 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.