سورة المعارج
Surat Al-Ma’arij kwa Kiswahili
Ngazi za Kupanda
- 70
- Aya 44
- Sura ya Makka
- Juzuu 29
- Kurasa 568–570
Surat Al-Ma’arij (المعارج) ni sura ya 70 katika Qur’ani na ina aya 44. Jina lake lina maana ya “Ngazi za Kupanda”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 29.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Ma’arij yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Ma’arij kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
سَأَلَ سَآئِلٌۢ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ١
Saala sailun biʿathabin waqiʿin
Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea!1
Maelezo
[1] Ameita, mwenye kuita, kuhimiza kama kufanya kejeli, iletwe upesi adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo hapana shaka itawashukia makafiri. -
لِّلْكَـٰفِرِينَ لَيْسَ لَهُۥ دَافِعٌ٢
Lilkafireena laysa lahu dafiʿun
Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia .2
Maelezo
[2] Wala hapana chochote cha kuzuia adhabu hiyo, -
مِّنَ ٱللَّهِ ذِى ٱلْمَعَارِجِ٣
Mina Allahi thee almaʿariji
Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja.3
Maelezo
[3] Kwani hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu, ambako huko ndiko zinatoka nguvu zinazo simama, na hukumu inayo tekelezwa. -
تَعْرُجُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيْهِ فِى يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُۥ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ٤
Taʿruju almalaikatu waalrroohu ilayhi fee yawmin kana miqdaruhu khamseena alfa sanatin
Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu!4
Maelezo
[4] Malaika na Jibrili wanapanda kwenda kunako toka amri yake kwa siku ambayo urefu wake ni miaka khamsini elfu kwa mujibu wa hisabu ya miaka ya duniani. -
فَٱصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا٥
Faisbir sabran jameelan
Basi subiri kwa subira njema.Hakika wao wanaiona iko mbali!5
Maelezo
[5] Basi, ewe Muhammad! Subiri uwastahamilie hizo kejeli zao, na kuhimiza kwao adhabu, kwa subira isiyo kuwa na mbabaiko ndani yake wala mashtaka. -
إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُۥ بَعِيدًا٦
Innahum yarawnahu baʿeedan
Hakika wao wanaiona iko mbali!6
Maelezo
[6] Hakika hao makafiri wanaiona hiyo Siku ya Kiyama ni kitu cha muhali kutokea. -
وَنَرَىٰهُ قَرِيبًا٧
Wanarahu qareeban
Na Sisi tunaiona iko karibu.7
Maelezo
[7] Na Sisi tunaona kuwa ni jambo jepesi katika uweza wetu, wala halina uzito wowote. -
يَوْمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلْمُهْلِ٨
Yawma takoonu alssamao kaalmuhli
Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa.8
Maelezo
[8] Siku mbingu itakapo kuwa kama fedha iliyo yayuka, -
وَتَكُونُ ٱلْجِبَالُ كَٱلْعِهْنِ٩
Watakoonu aljibalu kaalʿihni
Na milima itakuwa kama sufi.9
Maelezo
[9] Na milima itakapo kuwa kama sufi iliyo tiwa rangi na ikapigwa, -
وَلَا يَسْـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا١٠
Wala yasalu hameemun hameeman
Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake.10
Maelezo
[10] Wala jamaa hamuulizi jamaa yake: Nini hali yako? Kwa sababu kila mmoja kajishughulikia nafsi yake! -
يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ ٱلْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِى مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍۭ بِبَنِيهِ١١
Yubassaroonahum yawaddu almujrimu law yaftadee min ʿathabi yawmiithin bibaneehi
Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe,11
Maelezo
[11] Watakuwa wakijuulishana wao kwa wao mpaka wajuane baraabara, na ilhali hapana amuulizae mwenzie kitu. Kafiri atatamani lau ange pata kujikomboa nafsi yake na adhabu hiyo Siku ya Kiyama kwa kumtoa mwanawe awe ni fidia yake, -
وَصَـٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ١٢
Wasahibatihi waakheehi
Na mkewe, na nduguye,12
Maelezo
[12] Au mkewe, au nduguye, -
وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِى تُـْٔوِيهِ١٣
Wafaseelatihi allatee tuweehi
Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu,13
Maelezo
[13] Au jamaa zake aliyo khusiana nao, -
وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ١٤
Waman fee alardi jameeʿan thumma yunjeehi
Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye.14
Maelezo
[14] Na wote waliomo duniani, apate kuokoka yeye tu! -
كَلَّآ ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ١٥
Kalla innaha latha
La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa,15
Maelezo
[15] Ewe mkosefu! Wacha hayo unayo yatamani ya kutaka kujikomboa kwa fidia! Hakika huo moto, unawaka kweli! -
نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ١٦
Nazzaʿatan lilshshawa
Unao babua ngozi ya kichwa!16
Maelezo
[16] Utakubabua mikono yako, na miguu yako, na viungo vyako vyote, -
تَدْعُوا۟ مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ١٧
Tadʿoo man adbara watawalla
Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka.17
Maelezo
[17] Utanadi kwa jina la huyo aliye iacha Haki, na akaacha ut'iifu, -
وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰٓ١٨
Wajamaʿa faawʿa
Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi.18
Maelezo
[18] Na akakusanya mali akayaweka katika mabweta yake, wala hakutoa haki ya Mwenyezi Mungu iliomo katika hayo mali! -
۞ إِنَّ ٱلْإِنسَـٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا١٩
Inna alinsana khuliqa halooʿan
Hakika mtu ameumbwa na papara.19
Maelezo
[19] Hakika tabia ya binaadamu ni papara, mwingi wa kupapatika, -
إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعًا٢٠
Itha massahu alshsharru jazooʿan
Inapo mgusa shari hupapatika.20
Maelezo
[20] Na kutoridhika akifikiwa na lolote la karaha na uzito, -
وَإِذَا مَسَّهُ ٱلْخَيْرُ مَنُوعًا٢١
Waitha massahu alkhayru manooʿan
Na inapo mgusa kheri huizuilia.21
Maelezo
[21] Na ni mwingi wa kuzuia na kunyima akipata kheri na neema. -
إِلَّا ٱلْمُصَلِّينَ٢٢
Illa almusalleena
Isipo kuwa wanao swali,22
Maelezo
[22] Isipo kuwa wanao swali, -
ٱلَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَآئِمُونَ٢٣
Allatheena hum ʿala salatihim daimoona
Ambao wanadumisha Sala zao,23
Maelezo
[23] Ambao wanadumisha Swala zao, hawakikosi hata kipindi kimoja. -
وَٱلَّذِينَ فِىٓ أَمْوَٰلِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ٢٤
Waallatheena fee amwalihim haqqun maʿloomun
Na ambao katika mali yao iko haki maalumu24
Maelezo
[24] Na wale ambao katika mali yao ipo haki iliyo ainiwa -
لِّلسَّآئِلِ وَٱلْمَحْرُومِ٢٥
Lilssaili waalmahroomi
Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba;25
Maelezo
[25] iliyo wekwa kwa ajili ya masikini mwenye kuomba kutaka msaada, na anaye jizuilia kuomba pia. (Katika wanao zuilika kuomba wanaingia si wenye kustahi na kuona vibaya tu, bali pia wasio weza kuomba kama watoto wachanga, wagonjwa, na wanyama pia.) -
وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ٢٦
Waallatheena yusaddiqoona biyawmi alddeeni
Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo,26
Maelezo
[26] Na wale wanao isadiki Siku ya Malipo, basi wanajitayarisha kwa ajili yake; -
وَٱلَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ٢٧
Waallatheena hum min ʿathabi rabbihim mushfiqoona
Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi.27
Maelezo
[27] Na wale wanao iogopa adhabu ya Mola wao Mlezi basi wanajikinga nayo wala hawajitii katika jambo la kuwaletea adhabu hiyo. -
إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ٢٨
Inna ʿathaba rabbihim ghayru mamoonin
Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo.28
Maelezo
[28] Kwani hakika adhabu ya Mola wao Mlezi hapana hata mmoja anaye weza kuaminika nayo isimpate. -
وَٱلَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَـٰفِظُونَ٢٩
Waallatheena hum lifuroojihim hafithoona
Na ambao wanahifadhi tupu zao.29
Maelezo
[29] Na ambao wanazihifadhi tupu zao hata hawaemewi na matamanio yao. -
إِلَّا عَلَىٰٓ أَزْوَٰجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ٣٠
Illa ʿala azwajihim aw ma malakat aymanuhum fainnahum ghayru maloomeena
Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi30
Maelezo
[30] Lakini kwa wake zao na masuria wao hawazihifadhi; kwa sababu hapo hawalaumiwi kuifuata tabia ya maumbile. -
فَمَنِ ٱبْتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْعَادُونَ٣١
Famani ibtagha waraa thalika faolaika humu alʿadoona
Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka.31
Maelezo
[31] Basi mwenye kutafuta starehe ya maingiliano kwa wasio kuwa wake na masuria, basi hao tena ni wenye kuikiuka halali na kuingia katika haramu. -
وَٱلَّذِينَ هُمْ لِأَمَـٰنَـٰتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَٰعُونَ٣٢
Waallatheena hum liamanatihim waʿahdihim raʿoona
Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao,32
Maelezo
[32] Na hao wenye kuzihifadhi amana za sharia na amana za waja wa Mwenyezi Mungu, na walio lazimika nayo kwa Mwenyezi Mungu na kwa watu bila ya kukhuni wala kupunja, -
وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَـٰدَٰتِهِمْ قَآئِمُونَ٣٣
Waallatheena hum bishahadatihim qaimoona
Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao,33
Maelezo
[33] Na ambao kwa shahada zao wamesimama sawa sawa kwa haki bila ya kuficha wanalo lijua, -
وَٱلَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ٣٤
Waallatheena hum ʿala salatihim yuhafithoona
Na ambao wanazihifadhi Sala zao.34
Maelezo
[34] Na wanao hifadhi Swala zao wakizisali sawasawa kwa ukamilifu - -
أُو۟لَـٰٓئِكَ فِى جَنَّـٰتٍ مُّكْرَمُونَ٣٥
Olaika fee jannatin mukramoona
Hao ndio watakao hishimiwa Peponi.35
Maelezo
[35] Watu wenye sifa kama hizo nzuri watakuwa ni wenye kuhishimiwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu huko Peponi. -
فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ٣٦
Famali allatheena kafaroo qibalaka muhtiʿeena
Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu?36
Maelezo
[36] Kitu gani kinawapelekea hao walio kufuru kukujia mbio mbio ? -
عَنِ ٱلْيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ٣٧
ʿAni alyameeni waʿani alshshimali ʿizeena
Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto!37
Maelezo
[37] Kutoka kuliani na kushotoni kwa makundi? -
أَيَطْمَعُ كُلُّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ٣٨
Ayatmaʿu kullu imriin minhum an yudkhala jannata naʿeemin
Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema?38
Maelezo
[38] Je, kwani kila mmoja wao ana tamaa ya kuingia kwenye Pepo yenye neema, baada ya kusikia kuwa Mwenyezi Mungu amemuahidi Mtume wake na Waumini kuwatia Peponi? -
كَلَّآ ۖ إِنَّا خَلَقْنَـٰهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ٣٩
Kalla inna khalaqnahum mimma yaʿlamoona
La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua.39
Maelezo
[39] Basi nawaache hiyo tamaa yao ya kuingia Peponi. Hakika Sisi tumewaumba wao kutokana na maji ya kudharauliwa. -
فَلَآ أُقْسِمُ بِرَبِّ ٱلْمَشَـٰرِقِ وَٱلْمَغَـٰرِبِ إِنَّا لَقَـٰدِرُونَ٤٠
Fala oqsimu birabbi almashariqi waalmagharibi inna laqadiroona
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza40
Maelezo
[40] Naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote, na magharibi zote za siku, na sayari na hidaya, kwamba hakika bila ya shaka Sisi tuna uweza wa kuwaangamiza, -
عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ٤١
ʿAla an nubaddila khayran minhum wama nahnu bimasbooqeena
Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi.41
Maelezo
[41] Na kuwaleta walio wat'iifu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko wao. Wala Sisi hatushindwi kubadilisha huko. Huenda ikawa inakusudiwa kwa "mashariki zote" na "magharibi zote" ni maeneo ya mamlaka ya Mwenyezi Mungu yote ambayo hayana mpaka kama ilivyo ashiriwa katika Aya 137 ya Surat Al-A'araf: "Na tukawarithisha watu walio kuwa wanadharauliwa mashariki za nchi na magharibi zake ambayo tuliitia baraka", kuonyesha sehemu zote za hiyo nchi inayo tajwa. Na huenda ikawa makusudio yake ni mashariki za jua na mwezi na nyota zote na sayari, na magharibi zao, kwa ajili ya kuonyesha vile vile ufalme wa Mwenyezi Mungu wote. Na kwa hivyo inadhihirika kwetu kuwa vyombo vinavyo kwenda katika qubba la mbingu vinachomoza kwenye upeo wa mashariki na kuchwa kwenye upeo wa magharibi, au kwa uchache vinazunguka kutoka mashariki kwendea magharibi kuizunguka nyota ya Pole, katika sehemu ya kaskazini ya dunia. Kwani umbali wa Pole kwa nyota ni mdogo kuliko pahala unapo angalia, basi nyota hapo haichomozi wala haichwi, bali hupiga duru ndogo kuizunguka North Pole. Na kwa hiyo Aya inaashiria saa za usiku. Rejea kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na alama na kwa nyota wao wanaongoka." Na kwa udhaahiri wa kuchomoza na kuchwa ipo ishara ya kuzunguka kwa dunia, na hiyo ni neema kubwa kabisa katika neema za Mwenyezi Mungu juu ya maisha katika sayari hii. Kwani bila ya kuzunguka kwa dunia juu ya msumari-kati wake nusu ya dunia ingeli pigwa na jua mfululizo muda wa nusu mwaka kaamili, na ingeli nyimwa mwangaza kabisa nusu nyengine. Kwa hivyo uhai kama tulivyo uzoea usinge kuwako. Na tukifanya hizo mashariki na hizo magharibi ni za jua peke yake, wachilia mbali nyota nyengine na sayari, basi itakuwa ishara ni kule kuchomoza jua kila siku pahala pengine na kuchwa pahala pengine kila siku, au hata katika kila dakika linapo pita juu ya dunia. Kwani jua kila dakika linakuchwa pahala na linachomoza pahala papili mfululizo. Na haya ni katika mipango ya Mwenyezi Mungu na miujiza ya uweza wake. Tazama pia maoni ya wataalamu juu ya Aya ya 5 katika Surat Assaffat, na Aya 17 ya Surat Arrah'man. -
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا۟ وَيَلْعَبُوا۟ حَتَّىٰ يُلَـٰقُوا۟ يَوْمَهُمُ ٱلَّذِى يُوعَدُونَ٤٢
Fatharhum yakhoodoo wayalʿaboo hatta yulaqoo yawmahumu allathee yooʿadoona
Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa,42
Maelezo
[42] Basi waachilie wakiporojoka katika upotovu wao, na wakicheza na dunia yao, mpaka wakutane na siku yao waliyo ahidiwa kupewa adhabu. -
يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ ٱلْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ٤٣
Yawma yakhrujoona mina alajdathi siraʿan kaannahum ila nusubin yoofidoona
Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo,43
Maelezo
[43] Siku watakapo tolewa makaburini mbio mbio kumwendea huyo ataye waita, kama kwamba wamemweka ufundo na wakimuabudu duniani walivyo kuwa wakimkimbilia badala ya Mwenyezi Mungu, -
خَـٰشِعَةً أَبْصَـٰرُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمُ ٱلَّذِى كَانُوا۟ يُوعَدُونَ٤٤
Khashiʿatan absaruhum tarhaquhum thillatun thalika alyawmu allathee kanoo yooʿadoona
Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa.44
Maelezo
[44] Macho yameinama chini, hawawezi kuyanyanyua, yamegubikwa na unyonge na udhalili. Hiyo ndiyo siku waliyo kuwa wakiahidiwa duniani na wao wakiikanusha.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Ma’arij maana yake ni nini?
Al-Ma’arij maana yake ni “Ngazi za Kupanda”.
Surat Al-Ma’arij iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Ma’arij iko katika juzuu ya 29.
Surat Al-Ma’arij ina aya ngapi?
Surat Al-Ma’arij ina aya 44.
Surat Al-Ma’arij ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Ma’arij ni sura ya Makka.
Surat Al-Ma’arij ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 70 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.