Surat Al-Qalam (القلم) ni sura ya 68 katika Qur’ani na ina aya 52. Jina lake lina maana ya “Kalamu”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 29.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Qalam yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Qalam kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
نٓ ۚ وَٱلْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ١
Noon waalqalami wama yasturoona
Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo!1
Maelezo
[1] Nuun, ndio harufi ya N, iliyo anzia Sura hii ni kama kupinzana na hao wanao kadhibisha, na ili kuwazindua wenye kusadiki. Naapa kwa kalamu wanayo andikia Malaika na wenginewe, na hayo mambo ya kheri na manufaa wanayo yaandika, -
مَآ أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ٢
Ma anta biniʿmati rabbika bimajnoonin
Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu.2
Maelezo
[2] Hakika wewe, na Mwenyezi Mungu amekuneemesha kwa kukupa Unabii, si mchachefu wa akili, wala mpumbavu wa mawazo. -
وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ٣
Wainna laka laajran ghayra mamnoonin
Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika.3
Maelezo
[3] Na hakika unapata thawabu kubwa zisio katika kwa ajili ya kufikisha Ujumbe. -
وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ٤
Wainnaka laʿala khuluqin ʿatheemin
Na hakika wewe una tabia tukufu.4
Maelezo
[4] Na hakika wewe bila ya shaka umeshikamana na sifa nzuri kabisa na vitendo vizuri kabisa alivyo kuumba navyo Mwenyezi Mungu. -
فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ٥
Fasatubsiru wayubsiroona
Karibu utaona, na wao wataona!5
Maelezo
[5] Karibuni hivi, ewe Muhammad, utaona, na makafiri wataona, -
بِأَييِّكُمُ ٱلْمَفْتُونُ٦
Biayyikumu almaftoonu
Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu.6
Maelezo
[6] Ni nani kati yenu aliye mwenda wazimu. -
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ٧
Inna rabbaka huwa aʿlamu biman dalla ʿan sabeelihi wahuwa aʿlamu bialmuhtadeena
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka.7
Maelezo
[7] Hakika Mola wako Mlezi, Yeye ndiye Mwenye kumjua zaidi aliye iacha Njia yake, na Yeye ndiye Mwenye kuwajua zaidi wenye akili walio ongoka kumwendea Yeye. -
فَلَا تُطِعِ ٱلْمُكَذِّبِينَ٨
Fala tutiʿi almukaththibeena
Basi usiwat'ii wanao kadhibisha.8
Maelezo
[8] Basi usiyaache uliyo nayo ya kuwapinga wanao kanusha. -
وَدُّوا۟ لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ٩
Waddoo law tudhinu fayudhinoona
Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie.9
Maelezo
[9] Wanatamani lau ungeli kuwa laini kwao katika baadhi ya mambo, ili na wao wawe laini kwako, kwa tamaa upate kurudishiana nao. (Neno lililo tumiwa hapo "Tud- hinu fayud-hinuun", maana yake khasa "Upake mafuta na wao wapake mafuta". Kiswahili husema: Kumpaka mtu mafuta kwa mgongo wa chupa. Yaani kumpa sifa za uwongo, kumfanyia unaafiki. Kwa Kiarabu ni "Mudaahana". Kupakana mafuta) -
وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ١٠
Wala tutiʿ kulla hallafin maheenin
Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa,10
Maelezo
[10] Wala usiache mwendo wako ulio nao kwenda kinyume na kila mwingi wa viapo, mtu wa kudharauliwa, -
هَمَّازٍ مَّشَّآءٍۭ بِنَمِيمٍ١١
Hammazin mashshain binameemin
Mtapitapi apitae akifitini.11
Maelezo
[11] Mtapitapi mwenye kueneza aibu za watu, mwenye kuwasengenya watu, kuwasema kwa siri, mwenye kutwaa maneno baina ya watu kwa sababu ya kuwafisidi, -
مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ١٢
Mannaʿin lilkhayri muʿtadin atheemin
Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi,12
Maelezo
[12] Mwingi wa kupinga kila la kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi, -
عُتُلٍّۭ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ١٣
ʿUtullin baʿda thalika zaneemin
Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu.13
Maelezo
[13] Mgumu wa moyo, mwenye tabia ya ukavu, muovu maarufu kwa shari, juu ya sifa hizo mbovu alizo nazo. -
أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ١٤
An kana tha malin wabaneena
Ati kwa kuwa ana mali na watoto!14
Maelezo
[14] Ati kwa kuwa anajiona yeye ana mali na watoto wengi! Amezikadhibisha Aya zetu na amezipuuza. -
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ءَايَـٰتُنَا قَالَ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ١٥
Itha tutla ʿalayhi ayatuna qala asateeru alawwaleena
Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani!15
Maelezo
[15] Akisomewa Qur'ani husema: Hivi ni visa vya uwongo vya watu wa kale! -
سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلْخُرْطُومِ١٦
Sanasimuhu ʿala alkhurtoomi
Tutamtia kovu juu ya pua yake.16
Maelezo
[16] Tutambandika alama juu ya pua yake ya kumganda, apate kufedheheka mbele za watu. -
إِنَّا بَلَوْنَـٰهُمْ كَمَا بَلَوْنَآ أَصْحَـٰبَ ٱلْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا۟ لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ١٧
Inna balawnahum kama balawna ashaba aljannati ith aqsamoo layasrimunnaha musbiheena
Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi.17
Maelezo
[17] Sisi tumewafanyia mtihani watu wa Makka kwa kuwapa neema, nao wakazikufuru; kama tulivyo wafanyia mtihani hao watu wenye shamba, walipo chukua kiapo kuwa watakwenda vuna mazao ya shamba lao asubuhi mapema, -
وَلَا يَسْتَثْنُونَ١٨
Wala yastathnoona
Wala hawakusema: Mungu akipenda!18
Maelezo
[18] Wala wasimkumbuke Mwenyezi Mungu, wakafunganisha hilo jambo lao na kupenda kwake. -
فَطَافَ عَلَيْهَا طَآئِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَآئِمُونَ١٩
Fatafa ʿalayha taifun min rabbika wahum naimoona
Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala!19
Maelezo
[19] Basi ikaliteremkia shamba hilo balaa kubwa ilio toka kwa Mola wako Mlezi, na hali wao wamelala. -
فَأَصْبَحَتْ كَٱلصَّرِيمِ٢٠
Faasbahat kaalssareemi
Likawa kama usiku wa giza.20
Maelezo
[20] Likawa hilo shamba kama usiku wa giza kwa masaibu yalio lifikia. -
فَتَنَادَوْا۟ مُصْبِحِينَ٢١
Fatanadaw musbiheena
Asubuhi wakaitana.21
Maelezo
[21] Asubuhi wakawa wanaitana: -
أَنِ ٱغْدُوا۟ عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰرِمِينَ٢٢
Ani ighdoo ʿala harthikum in kuntum sarimeena
Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna.22
Maelezo
[22] Amkeni mapema mwende kondeni kwenu kama mmeazimia kuvuna. -
فَٱنطَلَقُوا۟ وَهُمْ يَتَخَـٰفَتُونَ٢٣
Faintalaqoo wahum yatakhafatoona
Basi walikwenda na huku wakinong'onezana,23
Maelezo
[23] Wakatoka, nao wakinong'ona kuambizana: -
أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا ٱلْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ٢٤
An la yadkhulannaha alyawma ʿalaykum miskeenun
Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni.24
Maelezo
[24] Msimwachie masikini yeyote kukuingilieni leo! -
وَغَدَوْا۟ عَلَىٰ حَرْدٍ قَـٰدِرِينَ٢٥
Waghadaw ʿala hardin qadireena
Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo.25
Maelezo
[25] Wakenda hapo asubuhi mpaka kwenye shamba lao, na azma yao ovu hiyo, na wao ni wenye uwezo kaamili wa kutenda hayo kwa kujigamba kwao. -
فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوٓا۟ إِنَّا لَضَآلُّونَ٢٦
Falamma raawha qaloo inna ladalloona
Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea!26
Maelezo
[26] Walipo liona limekuwa jeusi limeungua, walisema nao wamebabaika: Hakika sisi bila ya shaka tumepotea. Hili silo shamba letu! -
بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ٢٧
Bal nahnu mahroomoona
Bali tumenyimwa!27
Maelezo
[27] Bali ndilo shamba letu! Na sisi tumenyimwa! -
قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ٢٨
Qala awsatuhum alam aqul lakum lawla tusabbihoona
Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu?28
Maelezo
[28] Alisema aliye kuwa muadilifu wao na mbora wao akiwalaumu: Sikukwambieni mlipo kuwa mnasemezana kuwanyima masikini, hebu hamumkumbuki Mwenyezi Mungu mkaiacha niya yenu? -
قَالُوا۟ سُبْحَـٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَـٰلِمِينَ٢٩
Qaloo subhana rabbina inna kunna thalimeena
Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu.29
Maelezo
[29] Wakasema walipo rejea kwenye uwongozi wao: Tunamtakasa Mwenyezi Mungu kuwa katudhulumu kwa yaliyo tusibu. Hakika sisi wenyewe ndio tumejidhulumu kwa makusudio yetu maovu. -
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَـٰوَمُونَ٣٠
Faaqbala baʿduhum ʿala baʿdin yatalawamoona
Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao.30
Maelezo
[30] Wakawa wanaelekeana wao kwa wao wakilaumiana, -
قَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَـٰغِينَ٣١
Qaloo ya waylana inna kunna tagheena
Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka!31
Maelezo
[31] Wakisema: Huku ni kuhiliki kwetu! Hakika sisi tulikuwa tumepita mipaka katika dhulma zetu. -
عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ٣٢
ʿAsa rabbuna an yubdilana khayran minha inna ila rabbina raghiboona
Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.32
Maelezo
[32] Asaa Mola wetu Mlezi akatupa badala lilio bora kuliko hili shamba letu. Hakika sisi tunamtaka Mola wetu Mlezi peke yake atupe msamaha na malipo. -
كَذَٰلِكَ ٱلْعَذَابُ ۖ وَلَعَذَابُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ٣٣
Kathalika alʿathabu walaʿathabu alakhirati akbaru law kanoo yaʿlamoona
Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua!33
Maelezo
[33] Mfano wa kama hayo yaliyo yasibu hilo shamba ndio inakuwa adhabu yangu ninayo iteremsha duniani kwa anaye stahiki. Na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi lau kuwa watu wanajua hayo. -
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ٣٤
Inna lilmuttaqeena ʿinda rabbihim jannati alnnaʿeemi
Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi.34
Maelezo
[34] Hakika wachamngu watapata kwa Mola wao Mlezi Bustani za neema safi. -
أَفَنَجْعَلُ ٱلْمُسْلِمِينَ كَٱلْمُجْرِمِينَ٣٥
Afanajʿalu almuslimeena kaalmujrimeena
Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu?35
Maelezo
[35] Je! Sisi tudhulumu katika hukumu yetu, tuwafanye Waislamu sawa na makafiri? -
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ٣٦
Ma lakum kayfa tahkumoona
Mna nini? Mnahukumu vipi?36
Maelezo
[36] Vipi mnahukumia mfano wa hukumu kama hii ya dhulma? -
أَمْ لَكُمْ كِتَـٰبٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ٣٧
Am lakum kitabun feehi tadrusoona
Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?37
Maelezo
[37] Kwani mnacho kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu mnacho kisoma, -
إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ٣٨
Inna lakum feehi lama takhayyaroona
Kuwa mtapata humo mnayo yapenda?38
Maelezo
[38] Na humo yamo hayo mnayo yapenda? -
أَمْ لَكُمْ أَيْمَـٰنٌ عَلَيْنَا بَـٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۙ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ٣٩
Am lakum aymanun ʿalayna balighatun ila yawmi alqiyamati inna lakum lama tahkumoona
Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia?39
Maelezo
[39] Au kwani mnazo ahadi juu yetu zenye kutiliwa mkazo kwa viapo, zenye kubaki mpaka Siku ya Kiyama, kwamba mnayo haki ya hayo mnayo jihukumia? -
سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ٤٠
Salhum ayyuhum bithalika zaʿeemun
Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya?40
Maelezo
[40] Ewe Muhammad! Waulize washirikina: Ni nani dhamini wa hukumu hiyo? -
أَمْ لَهُمْ شُرَكَآءُ فَلْيَأْتُوا۟ بِشُرَكَآئِهِمْ إِن كَانُوا۟ صَـٰدِقِينَ٤١
Am lahum shurakao falyatoo bishurakaihim in kanoo sadiqeena
Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli.41
Maelezo
[41] Kwani wanao wanao shirikiana nao, na wanao fuata mwendo wao katika kauli yao hii? Basi na wawalete hao washirika wao, ikiwa wao ni wasema kweli katika madai yao. -
يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ٤٢
Yawma yukshafu ʿan saqin wayudʿawna ila alssujoodi fala yastateeʿoona
Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza,42
Maelezo
[42] Siku mambo yatapo shitadi na yakawa magumu, na wakatakiwa makafiri wasujudu kwa kuwaemea na kuwakejeli, na wasiweze, (Kuwekwa wazi mundi, ni kinaya ya kudhihirishwa kweli yote Siku ya kwima kondo, Siku ya Kiyama. Chambilecho Sayyid Abdulla bin Ali bin Nassir katika Al Inkishaf: Tafakari siku ya kwima kondo Ya kuaridhiwa kila kitendo Pindi madhulumu atapo ondo Achamba Ya Rabi namua naye) -
خَـٰشِعَةً أَبْصَـٰرُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ وَقَدْ كَانُوا۟ يُدْعَوْنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمْ سَـٰلِمُونَ٤٣
Khashiʿatan absaruhum tarhaquhum thillatun waqad kanoo yudʿawna ila alssujoodi wahum salimoona
Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima43
Maelezo
[43] Macho yao yameinama chini, yamefunikwa na fedheha. Na duniani walikuwa wakitakiwa wasujudu walipo kuwa wakiweza na wakakataa kusujudu. -
فَذَرْنِى وَمَن يُكَذِّبُ بِهَـٰذَا ٱلْحَدِيثِ ۖ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ٤٤
Fatharnee waman yukaththibu bihatha alhadeethi sanastadrijuhum min haythu la yaʿlamoona
Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua.44
Maelezo
[44] Ewe Muhammad! Nachilie na hao wanao ikadhibisha Qur'ani. Tutawajongeza kwenye adhabu kidogo kidogo kwa jiha wasio ijua kuwa adhabu itatokea huko. -
وَأُمْلِى لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِى مَتِينٌ٤٥
Waomlee lahum inna kaydee mateenun
Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara.45
Maelezo
[45] Na nitawapa muhula kwa kuiakharisha adhabu. Hakika mipango yangu ni ya nguvu, na hawezi kuporonyoka yeyote akasalimika nayo. -
أَمْ تَسْـَٔلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ٤٦
Am tasaluhum ajran fahum min maghramin muthqaloona
Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo?46
Maelezo
[46] Kwani wewe unawaomba ujira kwa kuufikisha Ujumbe wako, na kwa hivyo wao wanaona uzito kwa gharama hiyo unayo wakalifisha? -
أَمْ عِندَهُمُ ٱلْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ٤٧
Am ʿindahumu alghaybu fahum yaktuboona
Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika?47
Maelezo
[47] Au kwani wao wanajua yaliyo fichikana na wao wanayaandika na ndio wanahukumu kwa hayo? -
فَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ٤٨
Faisbir lihukmi rabbika wala takun kasahibi alhooti ith nada wahuwa makthoomun
Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa.48
Maelezo
[48] Basi wewe subiri kwa tunavyo wapa muhula na kukuakhirisha kukuletea manusura yetu juu yao. Wala usiwe kama Yunus, aliye mezwa na samaki, akawa na haraka na kuwaghadhibikia watu wake, alipo mnadia Mola wake Mlezi, naye kajaa hasira na ghadhabu, akitaka waadhibiwe kwa haraka. -
لَّوْلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ٤٩
Lawla an tadarakahu niʿmatun min rabbihi lanubitha bialʿarai wahuwa mathmoomun
Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa.49
Maelezo
[49] Lau kuwa neema ya Mola wake Mlezi haikumdiriki kwa kukubali toba yake, angeli tupwa kutokana na tumbo la samaki ufukweni, naye akiteseka kwa kuteleza kwake. -
فَٱجْتَبَـٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ٥٠
Faijtabahu rabbuhu fajaʿalahu mina alssaliheena
Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.50
Maelezo
[50] Lakini Mola wake Mlezi kamteuwa kwa kuikubali toba yake, na akamjaalia miongoni mwa watu wema. -
وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَـٰرِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا۟ ٱلذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجْنُونٌ٥١
Wain yakadu allatheena kafaroo layuzliqoonaka biabsarihim lamma samiʿoo alththikra wayaqooloona innahu lamajnoonun
Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.51
Maelezo
[51] Na makafiri wangeli karibia kukutelezesha na pahala pako, kwa jicho lao wanalo kuangalia kwa uadui na chuki wanapo isikia Qur'ani, wakisema: Hakika huyu ni mwendawazimu. -
وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَـٰلَمِينَ٥٢
Wama huwa illa thikrun lilʿalameena
Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.52
Maelezo
[52] Na Qur'ani si chochote ila ni mawaidha, na hikima, na ukumbusho kwa walimwengu wote.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Qalam maana yake ni nini?
Al-Qalam maana yake ni “Kalamu”.
Surat Al-Qalam iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Qalam iko katika juzuu ya 29.
Surat Al-Qalam ina aya ngapi?
Surat Al-Qalam ina aya 52.
Surat Al-Qalam ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Qalam ni sura ya Makka.
Surat Al-Qalam ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 68 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.