سورة الحاقة

Surat Al-Haqqa kwa Kiswahili

Tukio la Haki

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat Al-Haqqa (الحاقة) ni sura ya 69 katika Qur’ani na ina aya 52. Jina lake lina maana ya “Tukio la Haki”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 29.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Haqqa yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat Al-Haqqa kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. ٱلْحَآقَّةُ۝١

    Alhaqqatu

    Tukio la haki.1

    Maelezo
    [1] Kiyama ni Tukio litakalo tukia kwa haki, yaani kwa kweli.
  2. مَا ٱلْحَآقَّةُ۝٢

    Ma alhaqqatu

    Nini hilo Tukio la haki?2

    Maelezo
    [2] Nini hicho Kiyama kitacho tokea kweli?
  3. وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْحَآقَّةُ۝٣

    Wama adraka ma alhaqqatu

    Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki?3

    Maelezo
    [3] Na kitu gani kitacho kujuvya ukweli wake, na kitacho kupa sura ya kitisho chake na shida zake?
  4. كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌۢ بِٱلْقَارِعَةِ۝٤

    Kaththabat thamoodu waʿadun bialqariʿati

    Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha.4

    Maelezo
    [4] Kina Thamudi na kina A'di walikanusha Kiyama kinacho wagutua walimwengu wote kwa kitisho chake na shida zake.
  5. فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا۟ بِٱلطَّاغِيَةِ۝٥

    Faamma thamoodu faohlikoo bialttaghiyati

    Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.5

    Maelezo
    [5] Ama Thamudi basi walihilikiwa kwa tukio lilio pindukia mipaka yote kwa ukali wake.
  6. وَأَمَّا عَادٌ فَأُهْلِكُوا۟ بِرِيحٍ صَرْصَرٍ عَاتِيَةٍ۝٦

    Waamma ʿadun faohlikoo bireehin sarsarin ʿatiyatin

    Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika.6

    Maelezo
    [6] Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo ubaridi na mkali,
  7. سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَالٍ وَثَمَـٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًا فَتَرَى ٱلْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَىٰ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَةٍ۝٧

    Sakhkharaha ʿalayhim sabʿa layalin wathamaniyata ayyamin husooman fatara alqawma feeha sarʿa kaannahum aʿjazu nakhlin khawiyatun

    Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani.7

    Maelezo
    [7] Mwenyezi Mungu aliwasalitisha nao muda wa masiku saba, na siku nane zilizo fuatana mfululizo, utaona walio patikana na upepo huo wamekuwa maiti kama magogo ya mitende yaliyo kuwa matupu ndani yake. ("Masiku" ni wingi wa "Usiku"; "Siku" wingi wake ni "Siku" vile vile.)
  8. فَهَلْ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٍ۝٨

    Fahal tara lahum min baqiyatin

    Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki?8

    Maelezo
    [8] Je! Unamwona yeyote aliye bakia katika hao?
  9. وَجَآءَ فِرْعَوْنُ وَمَن قَبْلَهُۥ وَٱلْمُؤْتَفِكَـٰتُ بِٱلْخَاطِئَةِ۝٩

    Wajaa firʿawnu waman qablahu waalmutafikatu bialkhatiati

    Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia.9

    Maelezo
    [9] Akaja Firauni, na mataifa mengine yaliyo kufuru kabla yake, na wale jamaa walio acha mwendo wa haki na vitendo vya maumbile wakafanya vitendo vichafu kabisa hata miji yao ikapinduliwa juu chini.
  10. فَعَصَوْا۟ رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَةً رَّابِيَةً۝١٠

    Faʿasaw rasoola rabbihim faakhathahum akhthatan rabiyatan

    Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu.10

    Maelezo
    [10] Kila umma katika hawa walimuasi Mtume wa Mola wao Mlezi. Naye Mwenyezi Mungu akawashika kwa kuwaadhibu kwa mshiko ulio zidi ukali.
  11. إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلْمَآءُ حَمَلْنَـٰكُمْ فِى ٱلْجَارِيَةِ۝١١

    Inna lamma tagha almao hamalnakum fee aljariyati

    Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina,11

    Maelezo
    [11] Maji yalipo zidi ukomo wake, na yakapanda juu ya milima katika tukio la tofani ya Nuhu, Sisi tulikupandisheni, yaani kwa kuwapandisha wazee wenu wa asli, katika safina inayo kwenda baharini.
  12. لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةً وَتَعِيَهَآ أُذُنٌ وَٰعِيَةٌ۝١٢

    Linajʿalaha lakum tathkiratan wataʿiyaha othunun waʿiyatun

    Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi.12

    Maelezo
    [12] Ili kulifanya tukio hilo la kuwaokoa Waumini na kuwazamisha makafiri liwe zingatio na mawaidha kwenu, na lihifadhiwe na kila sikio lenye kuhifadhi linalo sikia.
  13. فَإِذَا نُفِخَ فِى ٱلصُّورِ نَفْخَةٌ وَٰحِدَةٌ۝١٣

    Faitha nufikha fee alssoori nafkhatun wahidatun

    . Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu,13

    Maelezo
    [13] Litakapo pulizwa barugumu kwa mpulizo mmoja,
  14. وَحُمِلَتِ ٱلْأَرْضُ وَٱلْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَٰحِدَةً۝١٤

    Wahumilati alardu waaljibalu fadukkata dakkatan wahidatan

    Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja,14

    Maelezo
    [14] Na ardhi na milima ikaondolewa pahala ilipo, na ikavunjwa mara moja,
  15. فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ ٱلْوَاقِعَةُ۝١٥

    Fayawmaithin waqaʿati alwaqiʿatu

    Siku hiyo ndio Tukio litatukia.15

    Maelezo
    [15] Siku hiyo ndiyo kitashuka cha kushuka,
  16. وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِىَ يَوْمَئِذٍ وَاهِيَةٌ۝١٦

    Wainshaqqati alssamao fahiya yawmaithin wahiyatun

    Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.16

    Maelezo
    [16] Na mbingu zitapasuka kwa kuondoka hukumu zake na sharia zake, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu baada ya kuwa madhubuti zenye nguvu.
  17. وَٱلْمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرْجَآئِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَـٰنِيَةٌ۝١٧

    Waalmalaku ʿala arjaiha wayahmilu ʿarsha rabbika fawqahum yawmaithin thamaniyatun

    Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi.17

    Maelezo
    [17] Na Malaika pembezoni mwake, na wapo Malaika wanane siku hiyo watakao beba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi, juu ya Malaika hawa wengine.
  18. يَوْمَئِذٍ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَىٰ مِنكُمْ خَافِيَةٌ۝١٨

    Yawmaithin tuʿradoona la takhfa minkum khafiyatun

    Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu.18

    Maelezo
    [18] Siku hiyo ndio mtaletwa kwa ajili ya kuhisabiwa. Wala haifichikani siri yenu yoyote mliyo kuwa mkiificha.
  19. فَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقْرَءُوا۟ كِتَـٰبِيَهْ۝١٩

    Faamma man ootiya kitabahu biyameenihi fayaqoolu haomu iqraoo kitabiyah

    Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!19

    Maelezo
    [19] Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema akiwatangazia furaha yake walio karibu naye: Chukueni msome kitabu changu!
  20. إِنِّى ظَنَنتُ أَنِّى مُلَـٰقٍ حِسَابِيَهْ۝٢٠

    Innee thanantu annee mulaqin hisabiyah

    Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.20

    Maelezo
    [20] Mimi nilikuwa na yakini tangu duniani kuwa nitapata hisabu yangu, basi nikajitayarisha nafsi yangu kwa mkutano huu.
  21. فَهُوَ فِى عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ۝٢١

    Fahuwa fee ʿeeshatin radiyatin

    Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza,21

    Maelezo
    [21] Basi huyo atakuwa katika maisha yaliyo enea kupendeza.
  22. فِى جَنَّةٍ عَالِيَةٍ۝٢٢

    Fee jannatin ʿaliyatin

    Katika Bustani ya juu,22

    Maelezo
    [22] Katika Bustani ya pahali na daraja ya juu.
  23. قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ۝٢٣

    Qutoofuha daniyatun

    Matunda yake yakaribu.23

    Maelezo
    [23] Matunda yake yakaribu kwa kuyachuma. (kuyatunda).
  24. كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَآ أَسْلَفْتُمْ فِى ٱلْأَيَّامِ ٱلْخَالِيَةِ۝٢٤

    Kuloo waishraboo haneean bima aslaftum fee alayyami alkhaliyati

    Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita.24

    Maelezo
    [24] Kuleni na mnywe kwa kula na kunywa kusio na karaha, wala maudhi, kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kwisha vitanguliza katika siku za duniani zilizo pita.
  25. وَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَـٰلَيْتَنِى لَمْ أُوتَ كِتَـٰبِيَهْ۝٢٥

    Waamma man ootiya kitabahu bishimalihi fayaqoolu ya laytanee lam oota kitabiyah

    Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu!25

    Maelezo
    [25] Ama mwenye kupewa kitabu chake kwa mkono wake wa kushoto atasema kwa majuto na huzuni: Laiti kuwa sikupewa kitabu changu,
  26. وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ۝٢٦

    Walam adri ma hisabiyah

    Wala nisingeli jua nini hisabu yangu.26

    Maelezo
    [26] Wala sikuijua hisabu yangu!
  27. يَـٰلَيْتَهَا كَانَتِ ٱلْقَاضِيَةَ۝٢٧

    Ya laytaha kanati alqadiyatu

    Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa.27

    Maelezo
    [27] Laiti kuwa kule kufa niliko kwisha kufa kungeli kuwa ndio kumalizika kwangu kwa mwisho, wala nisingeli fufuliwa tena!
  28. مَآ أَغْنَىٰ عَنِّى مَالِيَهْ ۜ۝٢٨

    Ma aghna ʿannee maliyah

    Mali yangu hayakunifaa kitu.28

    Maelezo
    [28] Hapana chochote nilicho kimiliki duniani kilicho nifaa.
  29. هَلَكَ عَنِّى سُلْطَـٰنِيَهْ۝٢٩

    Halaka ʿannee sultaniyah

    Madaraka yangu yamenipotea.29

    Maelezo
    [29] Uzima wangu umenipotea, na nguvu zangu zimenitoka.
  30. خُذُوهُ فَغُلُّوهُ۝٣٠

    Khuthoohu faghulloohu

    (Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu!30

    Maelezo
    [30] Wataambiwa walinzi wa Jahannamu: Mshikeni, na mfungeni mikono yake kwenye shingo yake.
  31. ثُمَّ ٱلْجَحِيمَ صَلُّوهُ۝٣١

    Thumma aljaheema salloohu

    Kisha mtupeni Motoni!31

    Maelezo
    [31] Kisha msimtie popote ila ndani ya Moto wa Jahannamu,
  32. ثُمَّ فِى سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَٱسْلُكُوهُ۝٣٢

    Thumma fee silsilatin tharʿuha sabʿoona thiraʿan faoslukoohu

    Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini!32

    Maelezo
    [32] Kisha mfungeni kwenye mnyororo mrefu kabisa.
  33. إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ ٱلْعَظِيمِ۝٣٣

    Innahu kana la yuminu biAllahi alʿatheemi

    Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu,33

    Maelezo
    [33] Hakika huyo alikuwa hamsadiki Mwenyezi Mungu Mtukufu,
  34. وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ۝٣٤

    Wala yahuddu ʿala taʿami almiskeeni

    Wala hahimizi kulisha masikini.34

    Maelezo
    [34] Wala hamhimizi yoyote kuwalisha masikini.
  35. فَلَيْسَ لَهُ ٱلْيَوْمَ هَـٰهُنَا حَمِيمٌ۝٣٥

    Falaysa lahu alyawma hahuna hameemun

    Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu,35

    Maelezo
    [35] Basi hii leo huyu kafiri hana jamaa wa kumtetea,
  36. وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ۝٣٦

    Wala taʿamun illa min ghisleenin

    Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.36

    Maelezo
    [36] Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni, ambao kwa hakika ni mchanganyiko wa damu na usaha.
  37. لَّا يَأْكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلْخَـٰطِـُٔونَ۝٣٧

    La yakuluhu illa alkhatioona

    Chakula hicho hawakili ila wakosefu.37

    Maelezo
    [37] Hawakili chakula hicho ila wakosefu walio kusudia kufanya maasi yao, na wakakamia kuendelea nayo.
  38. فَلَآ أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ۝٣٨

    Fala oqsimu bima tubsiroona

    Basi naapa kwa mnavyo viona,38

    Maelezo
    [38] Basi naapa kwa mnavyo viona katika vinavyo onekana,
  39. وَمَا لَا تُبْصِرُونَ۝٣٩

    Wama la tubsiroona

    Na msivyo viona,39

    Maelezo
    [39] Basi naapa kwa mnavyo viona katika vinavyo onekana, na msivyo viona katika ulimwengu wa ghaibu,
  40. إِنَّهُۥ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ۝٤٠

    Innahu laqawlu rasoolin kareemin

    Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima.40

    Maelezo
    [40] Kwamba hakika Qur'ani bila ya shaka inatoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ulimi wa Mjumbe mwenye cheo cha juu.
  41. وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تُؤْمِنُونَ۝٤١

    Wama huwa biqawli shaʿirin qaleelan ma tuminoona

    Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini.41

    Maelezo
    [41] Wala Qur'ani si maneno ya mtunga mashairi kama mnavyo dai. Ama nyinyi ni chache mno imani yenu ya kuwa Qur'ani inatoka kwa Mwenyezi Mungu.
  42. وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ۝٤٢

    Wala biqawli kahinin qaleelan ma tathakkaroona

    Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka.42

    Maelezo
    [42] Wala Qur'ani haisemi kwa maneno ya kumunyia munyia kama wanenavyo makuhani mlio wazoea. Ni uchache mno kukumbuka kwenu na kuzingatia khitilafu zilioko baina ya Qur'ani na maneno ya makuhani.
  43. تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ۝٤٣

    Tanzeelun min rabbi alʿalameena

    Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.43

    Maelezo
    [43] Hii ni uteremsho unao toka kwa Mwenye kuwaangalia walimwengu wote kwa kuwaumba na kuwalea.
  44. وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ ٱلْأَقَاوِيلِ۝٤٤

    Walaw taqawwala ʿalayna baʿda alaqaweeli

    Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu,44

    Maelezo
    [44] Na lau kuwa angeli dai kitu chochote ambacho tusicho kisema
  45. لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِٱلْيَمِينِ۝٤٥

    Laakhathna minhu bialyameeni

    Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia,45

    Maelezo
    [45] Basi bila ya shaka tungeli mshika akitoe kama mtu anavyo mkamata mtu kwa mkono wa kulia akammaliza hapo hapo.
  46. ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ ٱلْوَتِينَ۝٤٦

    Thumma laqataʿna minhu alwateena

    Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!46

    Maelezo
    [46] Kisha bila ya shaka tungeli mkata mshipa wake wa moyo, afe saa ile ile. (Biblia inasema katika Kumbukumbu la Torati 18.20 "Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa.")
  47. فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَـٰجِزِينَ۝٤٧

    Fama minkum min ahadin ʿanhu hajizeena

    Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia.47

    Maelezo
    [47] Na hapana yeyote katika nyinyi, hata ange kuwa na nguvu namna gani, angeli weza kuzuia adhabu yetu isimfikilie.
  48. وَإِنَّهُۥ لَتَذْكِرَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ۝٤٨

    Wainnahu latathkiratun lilmuttaqeena

    Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu.48

    Maelezo
    [48] Na hakika Qur'ani ni mawaidha kwa wanao fuata amri za Mwenyezi Mungu, na wanaepuka makatazo yake.
  49. وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ۝٤٩

    Wainna lanaʿlamu anna minkum mukaththibeena

    Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha.49

    Maelezo
    [49] Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba kati yenu wapo wanao ikanusha Qur'ani.
  50. وَإِنَّهُۥ لَحَسْرَةٌ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ۝٥٠

    Wainnahu lahasratun ʿala alkafireena

    Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa.50

    Maelezo
    [50] Na kwamba hakika hiyo bila ya shaka ni sababu ya majuto ya wanao ikataa, wakati watapo iona adhabu yao, na neema za wenye kusadiki.
  51. وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلْيَقِينِ۝٥١

    Wainnahu lahaqqu alyaqeeni

    Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.51

    Maelezo
    [51] Na hakika Qur'ani bila ya shaka ni Haki iliyo thibiti, isiyo na shaka yoyote.
  52. فَسَبِّحْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلْعَظِيمِ۝٥٢

    Fasabbih biismi rabbika alʿatheemi

    Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.52

    Maelezo
    [52] Basi mtakase Mola wako Mlezi, na dumisha kudhukuru jina lake.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat Al-Haqqa maana yake ni nini?

Al-Haqqa maana yake ni “Tukio la Haki”.

Surat Al-Haqqa iko katika juzuu ya ngapi?

Surat Al-Haqqa iko katika juzuu ya 29.

Surat Al-Haqqa ina aya ngapi?

Surat Al-Haqqa ina aya 52.

Surat Al-Haqqa ni ya Makka au ya Madina?

Surat Al-Haqqa ni sura ya Makka.

Surat Al-Haqqa ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 69 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.