سورة النصر

Surat An-Nasr kwa Kiswahili

Nusura

Msahafu

Mishary Rashid AlafasyPakua MP3Pakua PDF

Surat An-Nasr (النصر) ni sura ya 110 katika Qur’ani na ina aya 3. Jina lake lina maana ya “Nusura”. Ni sura ya Madina, iliyoteremshwa Madina baada ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.

Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat An-Nasr yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.

Surat An-Nasr kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

  1. إِذَا جَآءَ نَصْرُ ٱللَّهِ وَٱلْفَتْحُ۝١

    Itha jaa nasru Allahi waalfathu

    Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,1

    Maelezo
    [1] Ikithibiti nusura ya Mwnyezi Mungu na ushindi kwako na kwa Waumini,
  2. وَرَأَيْتَ ٱلنَّاسَ يَدْخُلُونَ فِى دِينِ ٱللَّهِ أَفْوَاجًا۝٢

    Waraayta alnnasa yadkhuloona fee deeni Allahi afwajan

    Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi,2

    Maelezo
    [2] Na ukawaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi,
  3. فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَٱسْتَغْفِرْهُ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ تَوَّابًۢا۝٣

    Fasabbih bihamdi rabbika waistaghfirhu innahu kana tawwaban

    Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba.3

    Maelezo
    [3] Basi mshukuru Mola wako Mlezi, na Sabbih' , Mtakase kwa sifa zake, na mtake akusamehe wewe na umma wako, kwani hakika Yeye ni Mwingi wa kupokea toba za waja wake. Maoni ya wataalamu juu ya Surat Annas'r:- Sura hii tukufu inaashiria kugomboka kwa Makka. Na sababu khasa iliyo pelekea kugomboka Makka ni Maqureshi walipo vunja mkataba wa amani wa Hudaibiya kwa kuwashambulia kabila ya Khuzaa', ambao walikuwa wana masikilizano na Mtume s.a.w., na wakawasaidia Bani Bakri katika hayo. Yalipo tokea hayo Mtume akaona waliyo yafanya Maqureshi kuvunja mapatano imembidi ende kuigomboa Makka. Basi akakusanya jeshi la nguvu lenye wapiganaji elfu kumi. Akenda mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa nane wa Hijra (Desemba mwaka 630 B.K.) Akawazuia watu wake wasipigane ila wakilazimishwa. Na Mwenyezi Mungu alipenda aingie Nabii na jeshi lake Makka bila ya vita. Na kwa hivi akapata ushindi mkubwa kabisa katika taarikhi ya wito wa Kiislamu, bila ya vita. Na Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola ya kwanza duniani bila ya vita na bila ya kumwagwa damu. Na huo ugombozi wa Makka ulikuwa na athari za kufikia mbali kwa pande za Dini na siyasa, kwani ilikuwa ni kuung'oa upagani, kuabudu masanamu, katika ngome yake kubwa, kwa kuvunjwa masanamu yaliyo simamishwa katika Al-kaaba, na yakaondolewa mapicha na masanamu yaliyo kuwemo. Na kwa kuingia Makka kwenye boma la Uislamu Nabii s.a.w. aliweza kuzishinda kabila zote zilizo bakia katika Hijazi, ambazo zilizo kuwa zina kani za kijahiliya, kama Hawazan na Thaqif. Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola si juu ya kabila wala nchi bali juu ya Imani, nayo ni Imani ya Kiislamu, na bendera ya Kiislamu

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Surat An-Nasr maana yake ni nini?

An-Nasr maana yake ni “Nusura”.

Surat An-Nasr iko katika juzuu ya ngapi?

Surat An-Nasr iko katika juzuu ya 30.

Surat An-Nasr ina aya ngapi?

Surat An-Nasr ina aya 3.

Surat An-Nasr ni ya Makka au ya Madina?

Surat An-Nasr ni sura ya Madina.

Surat An-Nasr ni sura ya ngapi katika Qur’ani?

Ni sura ya 110 katika Qur’ani.

Vyanzo

  • Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
  • Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
  • Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
  • Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
  • Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
  • Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.

Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.

Mipangilio ya kusoma

Fonti ya Qur’ani
Ukubwa wa Kiarabu
100%
Ukubwa wa tafsiri
100%
Mandhari

Ongeza kwenye skrini ya kwanza

ReadSurahFungua ReadSurah kutoka skrini ya kwanza, kwa skrini nzima. Sura ulizosoma hufunguka hata bila intaneti.

  1. Katika Safari, gusa kitufe cha kushiriki (Share). Kwenye iPhone mpya kiko kwenye menyu ya •••.
  2. Gusa “Add to Home Screen”. Huenda ukahitaji kusogeza chini.
  3. Gusa “Add”.