سورة المسد
Surat Al-Masad kwa Kiswahili
Kamba ya Makumbi
- 111
- Aya 5
- Sura ya Makka
- Juzuu 30
- Ukurasa 603
Surat Al-Masad (المسد) ni sura ya 111 katika Qur’ani na ina aya 5. Jina lake lina maana ya “Kamba ya Makumbi”. Ni sura ya Makka, iliyoteremshwa Makka kabla ya Hijra, na iko katika juzuu ya 30.
Katika ukurasa huu unaweza kusoma Surat Al-Masad yote kwa Kiarabu, pamoja na tafsiri ya Kiswahili ya Ali Muhsin Al-Barwani aya kwa aya na matamshi kwa herufi za Kilatini, na kusikiliza kisomo chake.
Surat Al-Masad kamili: Kiarabu, tafsiri ya Kiswahili na matamshi
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
تَبَّتْ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ وَتَبَّ١
Tabbat yada abee lahabin watabba
Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.1
Maelezo
[1] Imeteketea mikono ya Abu Lahab iliyo kuwa ikiwaudhi Waislamu, na yeye mwenyewe amehiliki pia. -
مَآ أَغْنَىٰ عَنْهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ٢
Ma aghna ʿanhu maluhu wama kasaba
Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.2
Maelezo
[2] Hayatolindwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu mali yake aliyo kuwa nayo, wala cheo chake alicho kichuma. -
سَيَصْلَىٰ نَارًا ذَاتَ لَهَبٍ٣
Sayasla naran thata lahabin
Atauingia Moto wenye mwako.3
Maelezo
[3] Ataingia katika Moto unao waka, aungue. -
وَٱمْرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلْحَطَبِ٤
Waimraatuhu hammalata alhatabi
Na mkewe, mchukuzi wa kuni,4
Maelezo
[4] Na ataingia pia kwenye Moto mkewe huyo aliye kuwa akibeba masengenyo baina ya watu, kama alivyo ingia yeye (mumewe). -
فِى جِيدِهَا حَبْلٌ مِّن مَّسَدٍۭ٥
Fee jeediha hablun min masadin
Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa.5
Maelezo
[5] Juu ya shingo yake itakuwa kamba ya mtende ya kumtesa.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Surat Al-Masad maana yake ni nini?
Al-Masad maana yake ni “Kamba ya Makumbi”.
Surat Al-Masad iko katika juzuu ya ngapi?
Surat Al-Masad iko katika juzuu ya 30.
Surat Al-Masad ina aya ngapi?
Surat Al-Masad ina aya 5.
Surat Al-Masad ni ya Makka au ya Madina?
Surat Al-Masad ni sura ya Makka.
Surat Al-Masad ni sura ya ngapi katika Qur’ani?
Ni sura ya 111 katika Qur’ani.
Vyanzo
- Arabic text: Tanzil Quran Text (Uthmani) (Tanzil Project, CC BY 3.0), reproduced without changes.
- Translation: Ali Muhsin Al-Barwani, from QuranEnc.com, version 1.0.1, reproduced without changes.
- Transliteration: Tanzil.net English transliteration.
- Recitation: Mishary Rashid Alafasy, via QuranicAudio.com and EveryAyah.com.
- Word by word: recordings and meanings from Quran.com (Quran Foundation), played when you tap a word.
- Madinah and IndoPak fonts (Settings): the text in those scripts and their fonts come from the Quran Foundation (Quran.com); the Madinah font is the King Fahd Glorious Quran Printing Complex's Uthmanic Hafs font.
Found a mistake? Report a mistake and we will check it against the source.